TANGAZO


Saturday, May 20, 2017

BALOZI SEIF IDDI AZUNGUMZA UFUNGUZI WA JUKWAA LA DUNIA LA UCHUMI JIJINI AMMAN, NCHINI JORDAN

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Rais wa Niger Bwana Mahamadou Issouton katika hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Mjini Amman Nchini Jordan lililofunguliwa na Kiongozi wa Nchi hiyo Mfalme Abdulla wa Pili. (Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)
Ujumbe wa Tanzania ukiwa miongoni mwa Viongozi walioshiriki Jukwaa la Uchumi la Dunia ambao wa kwanza kutoka kulia NI Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed
Aboud Mohamed.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mastacard  Bibi Tara Nathan akibadilishana mawazo na Ujumbe wa Tanzania unaoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Mkutano wa Jukwaa
la Uchumi la Dunia Mjini Amma Jordan.
Balozi Seif Kati kati katika picha ya pamoja na ujumbe wake mara baada ya kuwasilisha muelekeao wa Tanzania katika kuimarisha Utalii na fursa zinazopatikana kwa Taasisi zinazotaka kuwekeza miradi yao Tanzania  kwenye Mkutano wa Jukwaa la Uchumi la Dunia Mjini Amma Jordan.  
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika Warsha ya Sekta ya Utalii  ndani ya Jukwaa la Uchumi wa Dunia (World Economy Forum)  Mjini Amman Jordan alipokuwa akiwasilisha muelekeao wa Tanzania katika kuimarisha Utalii na fursa zinazopatikana kwa Taasisi zinazotaka kuwekeza miradi yao Tanzania.
Balozi Seif akibadilishana Mawazo na Waziri wa Mambo ya Nchi za nje wa Jordan Bwana Iman Safad mara baada ya ufunguzi wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Mjini Amma Nchini Jordan.  
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kiwa pamoja NA Viongozi wenzake wa Kimataifa walioshiriki ufunguzi wa Jukwaa la Dunia la Uchumi {WEF} Nchini Jordan. 
Balozi Seif na wadau wenzake wa Sekta ya Utalii kutoka nchi mbali mbali Duniani wakijibu Hoja za Washiriki wa Warsha ya Utalii iliyofanyika ndani ya Jukwaa la Uchumi la Dunia Nchini Jordan.

No comments:

Post a Comment