Kivuko kipya cha MV KAZI kikiwasili kwa mara ya kwanza upande wa Magogoni tayari kwa majaribio ya kubeba abiria na magari. (Picha zote na Alfred Mgeno - Temesa)
Magari yakiingia kwa mara ya kwanza kwenye kivuko
kipya cha MV KAZI tayari kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho
kilikua kikifanyiwa majaribio baada ya ujenzi wake kukamilika.
Abiria
wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa
Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara
ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.Abiria wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
Kivuko cha MV KAZI kikiondoka kwa mara ya kwanza kutokea Magogoni kuelekea Kigamboni kikiwa na abiria na magari. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio mara baada ya ujenzi wake kukamilika kabla ya kukabidhiwa kwa TEMESA.
Kivuko cha MV KAZI kikielea kwa mara ya kwanza majini huku kikiwa na abiria na magari, kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
Abiria wakishuka kutoka katika kivuko cha MV KAZI mara baada ya kuwasili upande wa Kigamboni kwa majaribio, ujenzi wa kivuko hicho umekamilika na kinategemewa kuanza kutoa huduma hivi karibuni.
Na Alfred Mgeno (Temesa)
KIVUKO cha MV KAZI hatimaye kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na magari kwa mara ya kwanza baada ya kukamilika kwa
matengenezo yake.
Majaribio hayo yalifanyika
kulingana na sheria na taratibu za vyombo vya majini ambayo inavitaka vyombo
vyote vya majini kufanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi ili viweze kupatiwa
cheti cha ubora “Seaworthiness Certificate”.
Awali wataalam kutoka Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI) waliweza kupima ubora na uimara wa kivuko hicho kwa
kutumia utaratibu wa kuweka mawe yenye kilo zinazolingana na uwezo wa kivuko
pamoja na magunia ya mchanga ili kuweza kupima uwezo wa kivuko kulingana na
mahitaji yaliyoainishwa kabla hakijabeba abiria na mizigo.
Zoezi hili pia
lilihusu kufanyika kwa kipimo cha kuhakikisha kuwa kivuko hakilali upande mmoja
yaani “Inclination test” ambapo kilionyesha Kivuko kiko sawa. Taarifa ya zoezi
hili itakuwa sehemu ya vitu vya makabidhiano wakati wa upokeaji wa Kivuko.
Miongoni
mwa waliokuwepo kushuhudia majaribio hayo alikuwa Mkuu wa Vivuko Magogoni/Kigamboni,
Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alisifu uwezo wa kivuko hicho na kuwataka
wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanakitunza kivuko hicho kwani kitawasaidia
kupunguza msongamano wa abiria na magari hasa majira ya asubuhi na jioni.
Ujenzi
wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa
kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170. Kivuko hicho kitakabidhiwa
rasmi hivi karibuni kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kuanza
kutoa huduma. Aidha ujio wa kivuko hicho utaongeza idadi ya vivuko kufikia vitatu
vitakavyotoa huduma ya kuvusha abiria na magari katika eneo la
Magogoni/Kigamboni.







No comments:
Post a Comment