Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya
mahakama alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo
jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Frank Shija – Maelezo)
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akiwasili katika viwanja vya mahakama kuhudhuria hafla ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akiwasili katika viwanja vya mahakama kuhudhuria hafla ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma (kushoto), akiwa pamoja na viongozi wenzake wakisubiri kumpokea mgeni rasmi katika maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe,Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
viongozi wa dini na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba wakati wa hafla ya
maaadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ripoti ya kesi za uchaguzi wa mwaka 2015 katika hafla ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa dini wakiomba wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa dini wakiomba wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia video ya makala fupi kuhusu mpango mkakati wa Mahakama iliyoonyeshwa mbele ya Rais Dkt. Magufuli wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya majaji
wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu wakiwa katika hafla ya maadhimisho ya
mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akikagua gwaride la Kikosi Maalumu cha Jeshi la Polisi nchini wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akipokea salamu ya utii kutoka kwa Kikosi Maalumu cha Jeshi la Polisi nchini wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjydcPI9ttj9_K5CR5bEcKNXhoIQWZRd8oye6ocnyPHcX_QTpYYpgOwsS1w228uC0szvz3o_eb-JHlPuri4zrN3nQFhBEAMhWwdOmct8uKkWaD9a93M9cBDvao7LJk_O5EQBxh_CyUHQi_l/s640/P11.jpg)
Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju (kushoto) walipokutana katika hafla ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya majaji pamoja na viongozi wa Serikali wakati wa hafla ya maadhimisho
ya mwaka mpya wa Mahakama leo jijini Dar es Salaam.Waliokaa kutoka kushoto ni
Jaji Mkuu wa Zanzibar Othmani Makungu, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.
Harrison Mwakyembe, Kaimu
Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Kiongozi Ferdinand
Wambali na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.
Na Beatrice Lyimo-Maelezo
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kukusanya Shilingi Trillioni 7.3 ambazo ni matokeo ya serikali kushinda kesi mbalimbali za ukwepaji kodi.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria na Mwaka mpya wa Mahakama iliyobeba kauli Mbiu isemayo Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.
Alisema kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi za pingamizi za kodi ambapo Serikali imeshinda kesi hizo japo fedha hizo hazijakusanywa mpaka sasa.
“Kukwepa au kutolipa kodi ni kosa kubwa sana, kila mtu anawajibu wa kulipa kodi nchini kwa maendeleo ya nchi” nalifafanua Dkt Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa katika kuelekea ukuaji wa uchumi, Mahakama iwe sehemu ya chanzo cha pato la taifa kwa kwa kuhakikisha wale wanaotakiwa kulipa fidia baada ya kushindwa kesi wanafanya hivyo pamoja na kuwabana wakwepa kodi kwani kutimiza hilo kutaleta mabadiliko katika uchumi wa nchi.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli alisema kuwa Maendeleo ya nchi hayaangalii chama chochote, hivyo amevitaka vyombo vya utoaji haki kutoa haki kwa usawa.
Kwa upande wake Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa Mahakama imeandaa Mpango mkakati uliolenga kufanya maboresho ndani ya Mahakama.
Alisema kuwa mpango mkakati huo umelenga masuala makuu matatu ikiwemo Utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, upatikanaji wa haki na kwa wakati, uimarishaji wa amani kwa wananchi na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama.
Aidha Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa Mahakama imefanikiwa kusikiliza mashauri ya kesi za uchaguzi kwa asilimia 100.
“Kati ya mashauri ya kesi 249 ikiwemo 53 za ubunge na 196 za madiwani ya waliopinga uchaguzi kati ya kesi hizo, kesi 52 za ubunge zilikamilishwa na kesi zote za madiwani zilikamilishwa” alifafanua Kaimu Jaji Mkuu.
Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Katiba imeanisha bayana Kanuni ambazo zinapaswa kuzingatiwa na Mahakama wakati ikitekeleza mamlaka yake ya utoaji haki.
“Utoaji haki mapema ipasavyo ni moja ya Kanuni ambazo Mahakama inapaswa kuzingatia katika utekelezaji wa majukumu yake kama inavyoelekezwa katika Katiba” alifafanua Mwanasheria Mkuu.
Alisema kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara katika nchi ya Tanzania hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Siku ya Sheria nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na Mahakimu ili kuweza kusikiliza kesi.
No comments:
Post a Comment