Mhandisi Mshauri anayesimamia ukarabati na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Mnara wa jengo la kuongozea ndege alipokagua ujenzi wa uwanja huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akitoa maelekezo kwa viongozi wa uwanja wa ndege wa Mwanza namna ya kushirikiana na Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group (BCEG) anayekarabati na kujenga uwanja huo.
Muonekano wa jengo
jipya la kuongozea ndege linalojengwa na kampuni ya Beijing Construction
Engineering Group (BCEG) katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi
anayejenga na kukarabati uwanja wa ndege
wa Mwanza Beijing Construction Engineering Group (BCEG), kuhakikisha ujenzi huo
unakamilika ifikapo Novemba mwaka huu.
Akizungumza
mara baada ya kukagua ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege, jengo la kuhifadhia
mizigo, eneo la kuegeshea ndege na jengo la umeme litakalotoa huduma katika
uwanja huo, Profesa Mbarawa amesema tayari Serikali imeshamlipa mkandarasi huyo
kiasi cha shilingi bilioni saba kwa ajili ya ujenzi huo.
“Sisi
tumeshamlipa pesa yake yote na hivyo tunachotaka kwake ni kukakamilisha kazi
yetu kwa wakati ili kuupa hadhi inayostahili uwanja wa ndege wa Mwanza amboa ni
kiungo muhimu katika kanda ya Ziwa”, Amesema Profesa Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amemuagiza Meneja wa uwanja wa ndege wa Mwanza Bi .Easter Madale
kuhakikisha vikwazo vyote vinavyomkabili mkandarasi vinaondolewa ili
kumuwezesha kufanya kazi kubwa kabla ya kipindi cha mvua za masika
zinazotarajiwa kuanza mwezi machi.
Kwa
upande wake Mhandisi Lili Ang
aneyesimamia ujenzi huo kutoka
kampuni ya BCEG amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa baada ya kupokea malipo wamejipanga
kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na viwango ili waweze kupata fursa nyingine za
ujenzi hapa nchini.
Naye
Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mwanza Bi .Easter Madale ameyataka mashirika ya
ndege kuongeza safari za ndege kwenye uwanja wa Mwanza kwa kuwa sasa utakuwa na
hadhi ya kimataifa na kusisitiza umuhimu wa wawekezaji wa hoteli, vituo vya
mafuta na maduka makubwa kuwekeza karibu
na uwanja huo ambao ndio lango la uchumi wa kanda ya ziwa.
Katika
hatua nyingine Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano ameelekea mkoani
Simiyu kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo amabapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa
kushiriki katika ufunguzi wa barabara ya Bariadi- Lamadi iliyojengwa kwa
kiwango cha lami.
Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawssiliano.

No comments:
Post a Comment