TANGAZO


Tuesday, January 24, 2017

MFANYABIASHARA WA MADINI KORTINI KWA KUMPIGA CHUPA MKEWE MBELE YA BABA MKWE

Na Woinde Shizza, Arusha

MFANYABIASHARA maarufu wa madini  jijini Arusha, Venance Moshi 
(30), amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi  mkewe kwa chupa usoni, wakiwa wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.

Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, mwendesha mashtaka wa Serikali, Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo, kuwa mnamo marchi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa yao, mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30), iliyomjeruhi vibaya.

Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo, kuwa hatua hiyo, ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadaye kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadaye kufikishwa mahakamani.

Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa  huyo alikana mashtaka ,na hakimu Msofe  alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande wa jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo.

Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016, upande wa jamhuri unatarajia  kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati ya polisi(PF3), hati ya daktari pamoja na picha za jeraha. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa february  6 ,mwaka huu ,saa tatu asubuhi.

Aidha katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo, Agnes Joseph anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo, waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho.

Alisema  ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio.

No comments:

Post a Comment