TANGAZO


Thursday, December 8, 2016

PROFESA MBARAWA ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA JICA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bi Suzuki Noriko (wa kawanza kulia), kuhusu maendeleo ya miradi ya ujenzi wa barabara nchini inayotekelezwa na shirika hilo.  Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bi Suzuki Noriko (wa kawanza kulia), walipokutana jjijini Dar es salaam leo. Kushoto kwa Makamu wa Rais wa JICA ni Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania Bw. Toshio Nagase. 
Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bi Suzuki Noriko, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa walipokutana  jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bi Suzuki Noriko (wa tatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wao mara baada ya kujadili mikakati ya kuboresha miundombinu nchini.(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)

No comments:

Post a Comment