Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na Kikundi cha Wawanawake cha Nia Njema cha Wete-Pemba, wakati wa mkutano huo na Viongozi wa Dini Kisiwani Pemba, uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Waumini madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo kisiwani Pemba wakati wa mkutano wake wa kutoa shukrani kwa ushirikiano wao katika shughuli na maendeleo na kudumisha amali Zanzibar na hafla ya uzindua Albam ya Kwanya ya Kikundi cha Kanisa la R.G.C, Chake-Chake Pemba iliozinduliwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji Pemba leo.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Waumini wa Dini wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo kisiwani Pemba wakati wa mkutano wake wa kuwashukuru kwa ushirikiano katika shughuli za maendeleo na kudumisha amani na kuwazinduliwa Albam ya Kwaya ya Kanisa la R.G.C, Chake-Chake, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji Pemba. kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na Mchungaji wa Kanisha la Anglikana Zanzibar, Emanuel Masoud.
Baadhi ya waumini wa madhehebu mbalimbali wa Dini ya Kikristo kisiwani Pemba wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar akitowa nasaha zake kwa waumini hao katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Pemba. Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungua Albam ya Kwaya ya Kanisa la T.G.C ya Nyimbo za kuitakia Amani Zanzibar uzinduzi huo umefanyika kastika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Pemba kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Zanzibar, Emanuel Masoud.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akionesha Albam ya Kwaya ya R.G.C ya Chakechake baada ya kuinduwa ikiwa na nyimbo za kuitakia Amani Zanzibar uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Pemba.

No comments:
Post a Comment