Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba katika mkutano na wananchi katika Kijiji cha Katarukila akiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Katurukila na kuwapongeza kwa kuwa Kijiji cha mfano kwa kuonyesha jitihada za dhati za kuhifadhi mazingira.
Bwana Candidius
Songela akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira January Makamba akingalia ramani inayo onyesha eneo lenye mgogoro
baina ya wanakijiji wa Katarukila na mwekezaji. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya
Kilombero Bw. James Ihunyo.
Na Lulu Mussa, Kilombero
WANANCHI wa Kijiji cha Katurulika, Wilaya ya Kilombero,
Mkoani Morogoro wameahidiwa Mifuko mia moja ya saruji ili kukamilisha ujenzi wa
zahanati katika tarafa yao inayohudumia
wakazi wa vijiji sita.
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. January Makamba ameahidi kutoa mifuko hiyo ndani ya wiki moja
ikiwa ni pongezi kwa Kijiji hicho kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi
mazingira na msitu wa Magombera.
Awali, Bwana Dandidius
Songela alimfamisha Waziri Makamba changamoto wanazokutana nazo katika Kijiji
chao kuwa, ni pamoja na mgogoro baina ya Kijiji cha Katarukila na mwekezaji
anayehodhi sehemu ya eneo la Kijiji na kusababisha uharibifu wa mazingira.
Waziri Makamba aliwasihi wanachi wa Kijiji cha Katarulika kuwa ni jukumu lao msingi kulinda msitu huo kwa nguvu zao zote na kubainisha kuwa Hifadhi
endelevu ya mazingira ndio mustakabali wa maisha yao.
Waziri Makamba ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) kumpa mwekezaji huyo "Restoration
Order" kwa mujibu wa Sheria ya
Mazingira ya mwaka 2004 kwa kumtaka arejesha
mazingira katika hali yake ya asili, kwakuwa ni eneo tengefu.
Kwa upande mwingine Waziri Makamba amemwagiza Mkurugenzi
wa Wilaya ya Kilombero Bw. Dennis Londo
kuhakikisha wanasheria wa Manispaa wanahudhuria kesi baina yao na mwekezaji
huyo bila kukosa kila inapotajwa na baada ya kuhumu kutolewa Waziri Makamba
ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza kwa
kina endapo kulikua na mianya yoyote ya rushwa katika mchakato wa kumilikisha
ardhi ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara.
Waziri Makamba yuko ziarani Kilombero kuangalia changamoto za
mazingira na awali alitembelea Mto Mkondoa Wilayani Kilosa.

No comments:
Post a Comment