Washiriki wa Miss Tanzania 2016 kutoka Kanda ya Mashariki wakiwa katika pozi.
Na Mwandishi wetu, Arusha
SHINDANO dogo la kumtafuta mrembo mwanamitindo TOP MODEL
limefanyika mkoani Arusha Jumamosi
iliyopita huku mrembo wa Sinza Sia Pius kutoka Kanda ya Kinondoni akiibuka
mshindi katika shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini
Arusha.
Jumla ya warembo 30 walipanda jukwaani kuwania taji hilo
ambalo ni la pili kushindaniwa kati ya
Mataji 5 yanayo shindaniwa kabla ya shindano kubwa la Fainali za Miss Tanzania
lililopangwa kufanyika jijini Mwanza tarehe 29 Oktoba 2016.
Washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wameingia
kambini tangu tarehe 30 Septemba 2016 jijini D’salaam , na baadae kuanza ziara
rasmi ya kutembelea mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha na kumaliza ziara yao
jijini Mwanza.
Wakiwa Makao Makuu ya Chama na Serikali mkoani Dodoma warembo hao 30 walishiriki katika shindano
dogo la kumtafuta mrembo anaevutia katika picha. (Miss Photogenic) ambapo
mrembo wa Dodoma Anna Nitwa aliibuka mshindi
katika shindano hilo akifuatiwa na Sia Pius kutoka Kanda ya Kinondoni.
Washindi hao 2 Miss Photogenic Anna Nitwa na Top Model Sia Pius tayari wamejipatia tiketi ya kuingia katika hatua ya
pili ya nusu Fainali (Top 15) huku mataji mengine 3 bado yanagombaniwa na
washiriki hao 30.
Mashindano hayo madogo yaliyobaki ni
Mrembo mwenye kipaji – Miss Talent
Mrembo mwanamichezo -
Top sports woman
Mrembo chaguo la watu – Miss Personality
Mataji hayo
madogo yote yatashindaniwa jijini Mwanza wiki hii kabla
ya Fainali za Taifa zilizopangwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2016. Katika ukumbi
wa Rock City Mall uliopo jijini Mwanza.





No comments:
Post a Comment