Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba, wa tatu kutoka kulia akiangalia chanzo cha maji kilichovamiwa katika Mto Mambogo.
Wananchi wa Kijiji cha Parakuyo wakisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba kabla ya kufanya mkutano wa hadhara kijijini hapo.
Wananchi wa Kijiji cha Parakuyo wakisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba kabla ya kufanya mkutano wa hadhara kijijini hapo.
Sehemu ya wananchi wa waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Parakuyo Wilayani Kilosa. Wananchi hao walimweleza Waziri (hayupo pichani) changamoto zinazowakabili juu ya Hifadhi ya mazingira.
Sehemu ya wananchi
wa waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Parakuyo Wilayani
Kilosa. Wananchi hao walimweleza Waziri (hayupo pichani) changamoto
zinazowakabili juu ya Hifadhi ya mazingira.
Na Lulu Mussa, Morogoro
WAZIRIwa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameitaka jamii ya
watu wa Parakuyo katika Wilaya ya Kilosa kuishi kwa amani, uvumilivu na upendo
miongoni mwao kwani ndio misingi ya watanzania.
Rai hiyo imetolewa leo
katika Mkutano wa hadhara uliojumuisha jamii za wakulima na wafugaji ambazo
zimekuwa na migogoro ya mara kwa mara. Waziri Makamba alizitaka jamii hizo
kuishi kwa amani na kuhifadhi mazingira kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.
Miongoni mwa changamoto
zilizobainishwa na jamii hiyo ni kutokuwa na elimu juu ya mabadiliko ya
Tabianchi na athari zake pamoja na kutokuwepo na matumizi bora ya ardhi.
Waziri Makamba ameuagiza
uongozi wa Wilaya na Kijiji kushirikiana pamoja kuunda kamati ya 'Amani'
itakayokuwa na wajumbe kutoka pande zote mbili za wakulima na wafugaji na
viongozi wa madhehebu ya dini ili kutafuta suluhu ya kudumu baina ya pande
mbili ambazo zimekua na migogoro ya mara kwa mara. "Undeni Kamati hii
mapema na Ofisi yangu itagharamia mafunzo kwa Kamati husika juu ya namna bora
ya kutatua migogoro" alisisitiza Waziri Makamba.
katika jitihada za kukuza
uelewa wa masuala ya mazingira na changamoto zake, Waziri Makamba ameitaka
Serikali ya Kijiji kuunda Kamati ndogondogo za Mazingira ambazo zipo kwa mujibu
wa sheria ya Mazingira na kuahidi kuipati mafunzo Kamati hizo ikiwa ni pamoja
na kutengeneza sheria ndogo ndogo zitakazotumika kama nyenzo ya kuhifadhi na
kusimamia Mazingira ya maeneo yao.
Aidha, Waziri Makamba
amesema kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ni muhimu sana na kuitaka jamii
ya Parakuyo na Twa twa twa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuhakiki na
kuhesabu mifugo yako ili kubaini ni ardhi kiasi gani inahitajika kwa wakulima
na kiasi gani kwa wafugaji. "ndugu zangu niwasihi, Serikali ina nia ya
dhati ya kuhakikisha kuna kuwa na matumizi bora ya ardhi, hivyo nawashauri
mmshiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupata uwiano wa idadi ya mifugo na
ardhi iliyopo" Makamba aliongezea.
Awali katika ziara ya
kikazi ya siku mbili Mkoani Morogoro Waziri Makamba pia alitembelea chanzo cha
maji na kujionea changamoto za kimazingira katika mto Mambogo.
No comments:
Post a Comment