TANGAZO


Monday, October 24, 2016

SIMBA ILIVYOIPIGA TOTO AFRICANS MABAO 3-0 MCHEZO WA LIGI KUU YA VODACOM UWANJA WA UHURU DAR ES SALAAM

Ubao wa matokeo ukionesha Simba bao 1 na Toto Africans 0. Hapa ikiwa ni mapumziko baada ya kumalizika kipindi cha kwanza katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Kipindi cha pili kikiwa kimeanza, mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu hizo. 
Mwinyi Kazimoto wa Simba akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Hamim Abdalla wa Toto Africans. 
Yussuf Mlipili wa Toto Africans akijaribu kuudhibiti mpira huku akifuatwa na Mohamed Ibrahim (Mo) wa Simba.
Yussuf Mlipili wa Toto Africans na Mohamed Ibrahim (Mo) wa Simba, wakiwania mpira wakati wa mchezo huo. 
Mavungo wa Simba pamoja na wenzake, wakishangilia bao aliloifungia timu yake, likiwa ni bao la pili kwa timu hiyo katika mchezo huo. 
Mavungo na Mzamiru, wote wa Simba, wakishangilia bao hilo.
Janvier Bukungu wa Simba akimtoka Sudi Mohamed wa Toto Africans katika mchezo huo. 
Golikipa wa Toto Africans akiudaka mpira wa kona uliopigwa kwenye lango lake. 
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la 3 lililofungwa na Mzamiru Yassin (katikati), katika mchezo huo na kuifanya Simba kumaliza mchezo huo na ushindi wa mabao 3-0. 
Mashabiki wa Simba wakishangilia bao hilo. 
Ubao wa matokeo ukionesha Simba mabao 3 na Toto Africans 0.

No comments:

Post a Comment