Mchungaji Samson Shango Donalds wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Semina ya kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry.
Waandishi
wa habari ya wakifuatili jambo wakati wa mkutano wao na Nabii Samson Rolinga wa
Kanisa la Omega Ministry leo Jijini Dar es Salaam.
Na Lilian Lundo - Maelezo
KANISA
la Omega Ministry of All Nations lenye makao yake Makuu Mbezi Afrikana, Jijini
Dar es Salaam limeandaa Semina ya Injili ya Neno la Mungu la kuiombea Taifa na Viongozi
wa Nchi, inayotarajiwa kufanyika Urafiki Nyangumi Jijini Dar es Salam Octoba 21
mpaka 23 mwaka huu.
Nabii
Samson Rolinga ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi
wa habari kuhusu Semina hiyo yenye lengo la kuiombea Taifa, Viongozi wa Nchi na
kuwafungua watu katika vifungo mbalimbali.
“TutaliombeaTaifa
lirudi katika misingi ya Mungu, vile vile tutawaombea watu waliofungwa na nguvu
za giza na magonjwa kama vile kanda, ukimwi na utasa,” alifafanua Nabii Rolinga.
Amesema
magonjwa yapo lakini pia yapo magonjwa ambayo yanatengenezwa na watu ilikumdhoofisha
mtu, hivyo katika semina hiyo kutafanyika maombi ya kuombea magonjwa hayo pamoja
na matatizo yote yanayotokonana roho za kurithi.
Vile
vile amesema kuwa kumekuwa na matatizo mengi sana ambayo watu hawana majibu ya
matatizo hayo mfano vijana wengi kutokuwa na kazi na kukata tama huku wakijraribu
kupambana na matatizo hayo kwa njia ya mwili.
Nabii
Rolinga amesema kuwa lengo lake nikuonyesha chanzo cha matatizo na kuyatatua kwa
njia ya maombi pamoja na kueleza namna ufalme wa giza unavyofanya kazi.
Kwa
upande wake Nabii Donald kutoka Mwanza amesema kuwa atakuwepo katika semina hiyo
ambayo itashughulikia matatizo ya Roho, kuvunja yanayoonekana katika ulimwengu wa
Roho pamoja na kuombea nchi na Utawala wa nchi.
Aidha
amesema kuwa watumishi wa Mungu wana jukumu kubwa la kuwaombea Viongozi wa Nchi
na Rais ili Mungu awasimamie katika majukumu yao ya kila siku ya
kuliongoza Taifa.
No comments:
Post a Comment