Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura akiongea na wawekezaji wa Makampuni matatu kutoka China leo 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia
Wambura akiongea na wawekezaji wa Makampuni matatu kutoka China leo 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam.
|
Baadhi ya wawekezaji wakifuatilia wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (hayupo pichani), alipozungumza nao leo 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya Viongozi na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na wawekezaji wakifuatilia mazungumzo hayo leo 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam.
|
Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)
NAIBU Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura amekutana na kufanya
mazungumzo na wawekezaji wa makampuni matatu kutoka China, lengo la ziara la
wawekezaji hao likiwa ni kufanya utafiti kujua ni namna gani Kampuni ya
StarTimes inapiga hatua katika kusaidia kukuza maendeleo katika sekta ya habari
Tanzania.
Katika mazungumzo hayo
yaliyofanyika leo Wizarani hapo, Mhe. Wambura amesema kuwa Serikali iko mbioni
kujenga Jengo Maalum kwa ajili ya shughuli za Kiutamaduni (Cultural Complex) ambalo linatarajiwa kujengwa Bagamoyo na ndani
ya jengo hilo kutawekwa vitu mbalimbali vinavyohusu utamaduni wa Tanzania.
Ameeleza kuwa, Tanzania imekuwa
ikishirikiana na China katika masuala mbalimbali yakiwemo ya michezo, utamaduni
na Sanaa ambapo baadhi wa wageni kutoka China wamekuwa wakifika kutalii na
kuwekeza, lakini pia baadhi ya Watanzania nao wamekuwa wakipata fursa ya
kutembelea China kujionea maendeleo na kujifunza mambo mbalimbali.
“Tanzania inapenda kushirikiana
na China katika mambo mbalimbali kama vile kutengeneza filamu, michezo na hata utamaduni,
kwakweli ushirikiano huu umekuwa wa manufaa kwetu sisi Watanzania kwani
unapanua wigo wa kukuza maendeleo”, alisema Mhe. Wambura.
Ameongeza kuwa, Kampuni ya StarTimes
ni moja kati ya Makampuni yaliyoisaidia Tanzania kuhama toka Analojia kwenda
Dijitali ambapo kampuni hiyo iliweza kuwekeza nchini kwa kuleta ving’amuzi
vyenye bei nafuu kiasi cha kumwezesha Mtanzania wa hali ya chini kumudu kununua
na kuweza kupata habari kupitia runinga yake.
Aidha, amewashauri wawekezaji hao
kutengeneza makala mbalimbali zinazohusu utamaduni wa Kitanzania kwa
kushirikiana na Watanzania kwani inaweza kuleta soko zuri ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Kiongozi wa
msafara wa wawekezaji hao ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Kampuni ya Star Media (T)
Ltd Bw. Leo amesema kuwa, China itaendeleza ushirikiano na Tanzania ambapo iko
mbioni kutoa nafasi kwa Watanzania kutoka Shirika la Utangazaji TBC na Wizara kwenda
kujifunza namna ya kutengeneza habari ikiwemo Makala na upigaji picha ili
taaluma hiyo ije kuwasadia wengine.
Mbali na kuja kutafiti namna
Kampuni ya StarTimes inavyofanya vizuri katika kuleta maendeleo Tanzania, ujio
wa wawekezaji hao nchini pia unafungua milango zaidi ya kibiashara baina ya
Tanzania na China na kuendeleza ushirikiano wenye lengo la kuleta maendeleo.
No comments:
Post a Comment