TANGAZO


Sunday, October 9, 2016

MKUU TEMESA AKATAA UZEMBE NA MAZOEA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU KWA WATUMISHIe

Mtendaji Mkuu TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (wa pili kushoto) akisikiliza Kaimu Meneja wa TEMESA Kagera Bw. Wilson Nyitwa(wa pili kulia) alipotembelea ofisi hiyo na kuzungumza na baadhi ya watumishi wa TEMESA Kagera kushoto ni Msaidizi wa Meneja wa TEMESA Kagera Bw. Charles Mbegete na kulia ni  Mhasibu Bi. Joviness Samson.(Picha na Theresia Mwami, TEMESA, Kagera)  
Mtendaji Mkuu TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (katikati) akikagua chumba maalumu kwa ajili ya injini (Engine Room) kulia ni msaidizi wa Meneja  Bw. Charles Mbegete na kushoto ni Kaimu Meneja TEMESA Kagera Bw. Wilson Nyitwa. 
Mtendaji Mkuu TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (wa tatu kushoto) akiongea na baadhi ya watumishi wa TEMESA Kagera alipotembelea kituoni hapo kukagua jinsi Ofisi inavyofanya kazi na kuzungumza na wafanyakazi.

Na Theresia Mwami TEMESA Kagera
MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu amewataka watumishi wake kuacha kufanya kazi kwa uzembe na mazoea badala yake waongeze ubunifu katika miundombinu iliyopo ili kuweza kuzalisha zaidi ikiwa ni sanjali na kuweka mikakati madhubuti ya kukusanya madeni siku hadi siku.

Ameota agizo hilo alipotembelea na kujionea hali ya karakana ya TEMESA mkoani Kagera na kumuagiza Kaimu Meneja wa TEMESA Kagera Bw.Wilson Nyitwa kusimamia kwa makini utekelezaji wa majukumu ya Wakala huo mkoani hapo.

“Inatupasa kuanza na hiki kidogo tulicho nacho kwa kuziba mianya ya uzembe na muongeze uadilifu na ufuatiliaji katika kazi tulizo nazo tufanikishe utendaji wa kazi zetu” alisema Dkt. Mgwatu.

Dkt Mussa Mgwatu ameongeza kuwa watendaji wanapaswa kupambana ili kulinda soko lililopo kwa sasa na hata kuongeza wateja zaidi. Kwa sasa wateja wa TEMESA ni taasisi za serikali ambazo zinapeleka magari na mitambo kutengenezwa katika karakana zao. 

Aidha kwa upande wake  Kaimu Meneja wa TEMESA Kagera Bw.Wilson Nyitwa alieleza kuwa Kituo chake  mbali na kuwa na karakana na kutengeneza magari na vifaa vya umeme,kukodishaji mitambo na usimikaji umeme katika majengo mbali mbali ya serikali pia kinasimamia uendeshaji wa vivuko viwili vilivyopo Kyanyabasa na Ruvuvu.

Alieleza kuwa TEMESA Kagera ina changamoto nyingi zikiwemo uchakavu wa Karakana yake iliyojengwa tangu mwaka 1958 pamoja na kukosa vitendea kazi muhimu pamoja na magari kwa ajili ya matumizi ya ofisi lakini bado wanafanya kazi kwa kujituma na kuzalisha zaidi ya Shillingi Million 50 kwa mwezi.

“Nakuomba Mtendaji Mkuu utusaidie gari moja kwa ajili ya matumizi ya kituo nyongeza ya mafundi, vitendea kazi vya kisasa vya karakana ,ukarabati wa karakana ya mkoa ili kutuwezesha kutekeleza majukumu yetu na kuzalisha zaidi.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi Kanda ya Ziwa na atatembelea vituo vya TEMESA vilivyopo ili kubaini changamoto na kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo na kwa kuanzia yupo Mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment