Mamia walijitokeza kushuhudia maonyesho ya urembo ya Mr na Ms Albino nchini Kenya. kila siku Albino wanakabiliwa na hatari ya kuwawa na viungo vyao vya mwili kuuzwa kutokana na imani za kishirikiana Afrika mashariki na Afrika kusini.
BBC
Akina dada walioshiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.
BBC
Malkia mpya! Louise Lihanda, aliyeshinda taji la urembo kwa akina dada atembea jukwani akiwa amevalia vazi la kupendeza lililotengenezwa kwa kutumia puto. Loiuse ambaye ni mwanafunzi, amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda taji hilo, katika mashindano yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
BBC
Wanaume walioshiriki katika mashindano hayo wasimama tisti jukwaani. walishiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.
BBC
Mfalme! Jairus Ongetta, ambaye amekabidhiwa taji ya uanamitindo bora kwa wanaume akiwa jukwaani na mavazi ya kupendeza.
BBC
Erick Thomas, awaongoza wanamitindo wenzake kwenye jukwaa wakati wa mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi. Lengo lake ni kuhakikisha kwamba watu walio na ulemavu huo wamejivunia ngozi yao.
BBC
Msichana huyu aliduwazwa na maonyesho hayo! Yeye ni miongoni mwa watu ambao kila siku wanakabiliwa na hatari ya kuwawa kutokana na imani za kishirikiana Afrika mashariki na Afrika kusini.
BBC
Miraba minne! John Ngatia, ambaye pia huwa anasakata densi, avalia sare ya mapigano ya ndondi katika maonyesho hayo, jijini Nairobi Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
BBC
Majaji walikuwa macho! Waliongozwa na mwanamitindo wa kimataifa Deliah Ipupa (katikati) tarehe 21Oktoba 2016.
BBC
Naomi Wafula, ajitokeza jukwaani akiwa amevalia vazi lililotengenezwa kwa sahani za plastiki katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
BBC
Mamia walihudhuria maonyesho hayo kuonyesha umoja wao na watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi katika mkahawa wa Carnivore jijini Nairobi Kenya, tarehe 21, Oktoba 2016
BBC
Amina makokha ajitokeza jukwaani akiwa amevalia sare ya mchezo wa raga katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
No comments:
Post a Comment