Ofisa Maendele ya Jamii Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Anna Muhina akiongea na Watoto (hawapo pichani) katika kongamano la mtoto wakike linaoendelea mjini Shinyanga.
Mkurugenzi wa Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Magereth Mussai akiongea na Watoto hawapo pichani katika kongamano la mtoto wakike linaoendelea mjini Shinyanga.
Na Mwandishi wetu, Shinyanga
KONGAMANO la mtoto wa kike lililofanyika leo mjini Shinyanga limeitaka
serikali kuweka juhudi za makusudi kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia hasa
kwa watoto wanaoozeshwa ndoa za utotoni kutoka kwa wazazi na walezi wao.
Maadhimisho haya yanaendelea kufanyika mjini Shinyanga ili kuungana na Nchi
Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike inayoendelea
kuadhimishwa Mkoani hapa ambayo kilele chake ni tarehe 11 Oktoba 2016.
Maadhimisho hayaufanyika kila mwaka ikiwa ni mwitikio wa Azimio la Umoja huo lililopitishwa mwezi
Desemba mwaka 2011.
Akiongea katika kongamano la watoto mkoani
shinyanga Mkurugenzi wa Watoto Bi. Magereth Mussai kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amelaani wale wote wanaoozesha
watoto ambao wako katika umri wa kwenda shule kwasababu ndoa za utotoni
uwafanya watoto hawa kushindwa kufikia ndoto zao ikiwemo haki ya kupata elimu
ya juu.
Wakati huo huo watoto wawili ambao hawakutaka
majina yao kutajwa kwasababu ya kulinda haki za watoto wametoa ushuhuda wao wa
ni namna gani ndoa za kulazimishwa wakiwa wadogo zilivyoelekea kukatiza ndoto
yao kabla ya kuokolewa na shirika la AGAPE kuwaokoa
na kuwaendeleza kielimu.
Mmoja wa Watoto hao ambaye jina limeifadhiwa
amesema ndoa yake ya utotoni iligubikwa na vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa
mme wake ambaye alimpatia ujauzito na baadae kumtelekeza yeye na mtoto.
Alendelea kusema kuwa inamuuma sana kama
mlengwa kuwa mzazi na wakati huo kuwa mwanafunzi anayesoma kwa msaada wa
mashirika yasiyo ya kiserikali huku baadhi ya wazazi na walezi wakiendeleza
vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Watoto wao kwa pamoja wameitaka serikali na
vyombo vya habari kuwekeza nguvu zao kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia
ikiwemo ndoa za utotoni ambazo zimekuwa kikwazo kwa mtoto wa kike kufikia ndoto
zake.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), inakadiriwa kuwa katika kipindi cha
miaka kumi ijayo wasichana wapatao milioni moja wanatarajiwa kuwa wameolewa katika
umri wa chini ya miaka 18 duniani kote.
No comments:
Post a Comment