TANGAZO


Saturday, September 10, 2016

Waislamu waanza Hija Saudi Arabia

Usalama mkali umedumishwa nchini Saudi Arabia

Image copyrightEPA
Image captionUsalama mkali umedumishwa nchini Saudi Arabia
Takriban Mahujaji wa kiislamu milioni 1.5 wamekusanyika nchini Saudi Arabia chini ya ulinzi mkali, kabla ya kuanza rasmi ibada ya hija ya kila mwaka.
Magari yamepigwa marufuku ya kukaribia msikiti mkuu, Grand Mosque, ambao ni eneo takatifu zaidi kwa waislamu, huku mahujaji wakifanyiwa ukaguzi na polisi katika vituo kadhaa kwenye eneo hilo.
Hija hii ni moja ya mikutano mikubwa zaidi ya kidini dunianiImage copyrightEPA
Image captionHija hii ni moja ya mikutano mikubwa zaidi ya kidini duniani
Zaidi ya mahujaji 2000 waliaga dunia mwaka jana wakati wa ibada ya hija, wengi wao wakiwa raia wa Iran.
Iran iliilaumu Saudi Arabia kwa kutosimamia ibada za Hija inavyofaa, na imekataa kuwaruhusu raia wake kuenda Saudi Arabia kuadhimisha ibada ya Hija.
Hija hii ni ya kuimarisha undugu katika dini ya kiislamuImage copyrightEPA
Image captionHija hii ni ya kuimarisha undugu katika dini ya kiislamu

No comments:

Post a Comment