Na Daudi Manongi, Maelezo,Dar es Salaam
15.9.2016
TAKWIMU zilizotolewa
na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza imeonyesha kuwa asilimia 96 ya
wananchi wanakubali hatua za kiutendaji kazi za Rais John Pombe Magufuli ikiwemo
uondoaji wa wafanyakazi hewa na sera ya elimu bure.
Taarifa iliyotolewa leo
katika vyombo vya habari na Mshauri Mwandamizi wa Mawasiliano wa Twaweza, Risha
Chande alisema asilimia 88 ya wananchi wana imani kuwa Rais Magufuli ataendelea
na kasi aliyoanza nayo mpaka mwisho wa awamu yake ya kwanza ya uongozi.
“Utafiti huu
unaonyesha kuwa asilimia 69 ya wananchi walifuraishwa na juhudi za Rais za
uondoaji wa wafanyakazi hewa, wakati
asilimia 61 walipongeza sera ya elimu bure wakati asilimia 61 walifurahishwa na
usimamishwaji wa watumishi wa serikali” alisema Chande.
Chande alisema kuwa katika
utafiti huo unaonyesha wananchi wengi kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali
ya awamu ya tano ya kufanya maboresho katika huduma za umma ikiwemo mamlaka ya mapat (asilimia 85), mashuleni
(asilimia 75),vituo vya polisi (asilimia 74),mahakama (asilimia 73), vituo vya
afya (asilimia 72).
Aliongeza kuwa kwa
upande wa huduma zinazotolewa katika utumishi wa umma, utafiti unaonyesha kuwa asilimia
95 ya wananchi wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na madaktari, walimu, na
maofisa tawala katika ofisi za umma.
“Pamoja na kiwango
kikubwa cha kukubalika kwa Serikali ya wamu ya Tano wananchi wamesema suala la umakini
na kanuni za demokrasia na haki ni vyema zifuatwe ambapo wananchi nane kati ya kumi wanasema watendaji
waondolewe pale tu panapokuwepo udhibitisho wa vitendo viovu” alisema Chande.
Akifafanua zaidi
Chande alisema utafiti huo pia umeonyesha kubadilika kwa matarajio ya wananchi ambapo
katika kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya kutojali miongoni mwa wananchi kulikotokana na utendaji duni kutoka kwa
watendaji.


No comments:
Post a Comment