TANGAZO


Friday, August 26, 2016

Udhaifu mkubwa wagunduliwa simu za iPhone

Ahmed Mansoor

Image copyrightAP
Image captionUjumbe ulitumwa kwa mwanaharakati wa haki za binadamu Ahmed Mansoor
Mfumo wa Apple wa utendaji wa iOS umegundulika ambao utawezesha kupachikwa kwenye kifaa cha uchunguzi kukiwezesha kubofya kwenye kiunganishi.
Uvumbuzi huo ulifanyika baada ya wakili anayetetea haki za kibinadamu kutoa taarifa kwa watafiti wa masuala ya usalama kuhusu jumbe alizozipata bila kutarajia.
Waligundua taarifa nyingine tatu za awali zisizofahamika zilizovuja kutoka kwa mfumo wa Apple .
tangu wakati huo Apple imetoa taarifa ya kuelezea tatizo hilo na namna linavyoshughulikiwa na kampuni hiyo.
Makampuni mawili ya usalama yaliyohusika , Citizen Lab na Lookout, yamesema yamehifadhi taarifa hizo za uvumbuzi hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.
Kampuni ya Citizen Lab inasema , simu yake ya iPhone 6 ingekuwa ''imefunguliwa'' , ikimaanisha mfumo mwingine ambao haukuidhinishwa ungelikuwa umewekwa kwenye simu yake.
"Na kama simu yake ingeathiriwa , ingekuwa kifaa cha upelelezi cha digitali ndani ya mfuko wake wa nguo, yenye uwezo wa kung'amua taarifa kwa kutumia kamera na kipaza sauti cha simu kurekodi simu zake za WhatsApp na Viber , kuingia kwenye jumbe alizotuma kwa simu na kuweza kumfuatilia kote anakoenda," ilisema kampuni ya Citizen Lab.
"Hatuna taarifa zozote za matukio ya aina hii ya iPhone suala linalofanya tukio hili kuwa la nadra ."
Watafiti wanasema wanaamini mfumo huu wa uchunguzi unaohusisha spyware ulibuniwa na kampuni ya NSO Group, ya Israel ya ''vita vya mitandaoni"

No comments:

Post a Comment