Khamisi Mussa
HUDUMA ya usafiri wa treni kati ya kituo cha Stesheni cha jijini Dar es Salaam na kituo cha Pugu imeanza rasmi kutolewa jana kwa ajili ya kupunguza shida ya usafi kwa wakazi wa maeneo hayo.
Safari ya kwanza ya treni hiyo, ilianza katika kituo cha stesheni katikati ya jiji saa 3 asubuhi kuelekea kituo cha Pugu na kwamba safari hiyo itakuwa ikitolewa mara 3 kwa siku.

Usafiri huo, unategemewa kusaidia mbali na kuwahi kazini lakini pia kuongeza kipato kwa wakazi wa maeneo hayo, ambao wanategemea sana mazao ya kilimo katika maisha yao.
Wengi wa wakazi wa maeneo ya Pugu wanafanya uchuuzi wa mboga mboga na mihogo, na hivyo kwa kuanza safari hizo, zinategemewa kuwasaidia sana katika ubebaji wa mizigo yao hiyo, ambayo ilikuwa ikiwasumbua sana katika usafiri waliokuwa wakiutumia, usafiri wa daladala hadi kusababisha kuchelewa kufanyabiashara zao na wakati mwingine kukataliwa kupanda gari hizo kutokana na mizigo waliyokuwa wakiibeba.
Wakati mwingine kulazimishwa kulipa gharama kubwa jambo lililokuwa likiwapunguzia kipato cha biashara zao hizo.
Baadhi ya abiri walioulizwa kuhusu faida ya kuwepo kwa huduma ya treni hiyo, walisema kuwa itawasaidia kuokoa fedha nyingi walizokuwa wakichajiwa na watoa huduma za daladala na pia itawasaidia kuwa kwenye shughuli zao za biashara na pia kuwahi kurudi majumbani kwao.

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakigombania kupanda katika mabehewa baada ya kuanzishwa usafiri huo.
Abiria wakiwa kwenye treni hiyo, kuelekea Pugu.
Abiria wakipanda treni hiyo, kuelekea Pugu.
Wanafunzi
wa Shule Mbalimbali wakiwa ndani ya mabehewa ya Treni ya Kampuni ya
Reli (TRL) katika Stesheni ya Dar es Salaam kwenda Pugu huduma ambayo
imeanza kutolewa .
Abiria wakipatiwa maelekezo kutoka kwa Ofisa wa Polisi kabla ya kupanda kwenye treni hiyo, kuelekea Pugu.
Abiria wakiwa ndani ya treni kuelekea Pugu.

No comments:
Post a Comment