Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Mhe. Anthony Mavunde akisisitiza umuhimu wa wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia jitihada za Serikali kuwawezesha Vijana kiuchumi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajiara na Wenye ulemavu.
Baadhi ya
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Mhe. Anthony Mavunde na waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam, kuhusu maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani itakayoadhimishwa Kitaifa, tarehe
14/10/2016, Mkoani Simiyu.
Na Frank
Mvungi-Maelezo
RAIS wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa
Mgeni rasmi siku ya Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kitaifa
yatakayofanyika Mkoani Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.
Kauli hiyo
imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi
Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari.
Mhe. Mavunde
amebainisha kuwa Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini
kwa uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.
Akifafanua
kuhusu kauli mbiu hiyo Mhe. Mavunde amesema lengo la kauli mbiu hii ni
kuzihimiza nchi wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu Vijana
katika shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi
ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na Nishati ili kufikia
shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 20130.
Akizungumzia
maadhimisho hayo Kitaifa Mhe . Mavunde amesema kuwa vijana watapata fursa ya
kushiriki shughuli mbalimbali kama makongamano,
matamasha, michezo, maonnyesho ya
Kazi za Vijana, Shughuli za kujitolea na maandamano ya amani.
“Tanzania
tutasherekea siku ya Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele
kitakuwa tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hii itaenda sambamba na
Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage
Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka
2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Wazo la kuwa
na siku ya Vijana Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa
mwaka 1991 Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta njia ya kuchangisha
fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000 nchi wanachama wa
Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku ya Vijana Duniani
kulingana na mazingira yake kwa kuzingatia kauli mbiu ambayo huandaliwa na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

No comments:
Post a Comment