TANGAZO


Wednesday, July 27, 2016

WIZARA OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU, BUNGE NA WATU WENYE ULEMAVU KUHAMIA DODOMA WIKI IJAYO

Mkurugenzi wa Utawala na Raslimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu, Issa Nchasi akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri Jenista Mhagama na Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi-Utawala, Samwel Mwashambwa. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea leo jijini Dar es Salaam na Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma, Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Dr. Abdallah Possi. 
Baadhi ya Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Jenista Mhagama wakati wa kikao kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma.

No comments:

Post a Comment