Kaimu Mkuu wa Mkoa Pwani Bw.Shangwe Twamala akitoa taarifa maendeleo ya kisekta kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (katikati) alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapo leo Mjini Kibaha.
Afisa Tawala Wilaya ya Kibaha Bi. Sozy Mgate akieleza changamoto za sekta ya michezo kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (wa kwanza kushoto) alipofanya ziara ya kikazi leo Mjini Kibaha kujionea maendeleo ya kisekta katika Mkoa huo.
Mwakilishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki Mhandisi Christopher John akitoa ufafanuzi kuhusu kukosekana kwa usikivu wa matangazo katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani kwa Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi Mjini Kibaha,Mkoani Pwani kwa lengo la kujua maendeleo ya kisekta katika mkoa huo.
Mbunge wa Viti Maalum Pwani Mhe.Hawa Mchafu akimshukuru Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (wapili kushoto) kwa kutembelea Mkoa wa Pwani leo na kujionea changamoto za kisekta zinazohusu Wizara yake.
Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Mkoa wa Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (watatu kushoto) alipofanya ziara ya kikazi Mjini Kibaha leo kujionea maendeleo ya sekta kwa wizara yake, (wapili kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa Bw.Shangwe Twamala na (wapili kulia) Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Hawa Mchafu.
Baadhi ya Maafisa Habari,Maafisa Michezo,Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (watatu kushoto) alipofanya ziara ya kikazi leo Mjini Kihaba,Mkoani Pwani kujua maendeleo ya sekta kwa wizara yake , (wapili kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa Bw.Shangwe Twamala na (wapili kulia) ni Mbunge wa Viti Maalum Pwani Mhe. Hawa Mchafu.
Na Anitha Jonas –
MAELEZO
Tarehe 09/07/2016
WATENDAJI wa Mkoa wa
Pwani watakiwa kuwa wawazi kwa waandishi
wa habari pale wanapotaka kupata taarifa
kutoka kwao.
Hayo yamesemwa leo Mjini
Kibaha, Mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura alipofanya ziara ya
kikazi mkoani hapo kufuatilia utekelezwaji wa maendeleo ya kisekta kwa wizara
yake.
“Kwa kuwapa
ushirikiano wakutosha waandishi wa habari kutasaidia kuepuka kuandikwa kwa
habari zisizona taarifa kamili ambazo huleta mkanganyiko kwa jamii na kuharibu
taswira ya ofisi, hivyo ni vyema mshirikiane nao”,alisema Naibu Waziri Wambura.
Pamoja na hayo Mhe.
Naibu Waziri aliangiza kuwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017 Kitengo cha Habari
kipewe kipaumbele na kitengewe bajeti
itakayokidhi mahitaji pamoja na
kununuliwa vitendea kazi ili kurahisisha
utekelezaji wa majukumu yao kwa urahisi ikiwa ni pamoja na kutangaza shughuli za
maendeleo ya Mkoa.
Kwa upande wa Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bw.Shangwe Twamala alisema mkoa huo unakabiliwa na
changamoto ya uhaba wa Maafisa Michezo kwa baadhi ya Wilaya pamoja na Maafisa
Utamaduni ila suala hilo kwasasa limeshawasilishwa kwa ngazi husika na wanalifanyia
kazi.
Pamoja na hayo Kaimu
wa Mkoa huyo aliendelea kusema Mkoa huo unakabiliwa pia na changamoto ya
usikivi wa matangazo ya Redio na Televisheni kwa baadhi ya maeneo kama
Rufiji,Mafia na mengineyo.
Naye Kaimu Meneja wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki Bw. Bernard Haule
alitoa ufafanuzi kuhusu suala la kukatwa kwa matangazo katika chaneli zote pale
malipo yanapoisha katika ving’amuzi vya Azam na Zuku kwa kusema leseni zao ni
tofauti na zile za Startimes na Continental ambazo mbali na malipo ya kifurushi
yanapokwisha wao bado huonyesha chaneli tano za taifa bure ambazo ni ITV, Star
Tv, Channel Ten, EATV na TBC 1.
Pamoja na hayo
Mhe.Wambura aliagiza kuwa watendaji wahakikisheni wanatenga maeneo ya viwanja vya michezo yasiyo na mgogoro kwani michezo ni ajira na inasaidia vijana
kujikwamua kiuchumi,hivyo ni vyema ipewe kipaumbele.
Halikadhalika Naibu
Waziri Wambura alitoa wito kwa wasanii Muziki wa Mkoa wa Pwani kuiga mfano wa marehemu Baraka Mwishehe kwa kutunga nyimbo zenye
maadili na zenye kubeba ujumbe wa kuelimisha na kuburudisha jamii.
Hata hivyo Naibu
waziri aliendelea kuwasisitiza watanzania wote kwa ujumla kuenzi lugha ya
Kiswahili kama yanavyofanya mataifa mengine duniani kuenzi lugha zao mfano
China.

No comments:
Post a Comment