Baadhi ya askari
wakitoa heshima wakati wimbo wa taifa unaimbwa kabla ya uzinduzi wa Mpango wa
Usalama wa Jamii unaosimamiwa na Jeshi la Polisi nchini leo jijini
Dar es
salaam.
|
Kikundi cha Jeshi la
Polisi wakitumbuiza kwa ngoma ya “makirikiri” uzinduzi wa Mpango wa Usalama wa
Jamii unaosimamiwa na Jeshi la Polisi nchini leo jijini
Dar es Salaam.
|
Moja ya vituo vya
Polisi vinavyohamishika ambacho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli amekizindua jijini Dar es Salaam.
|
Na Jonas
Kamaleki
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
amelitaka jeshi la polisi nchini kuwadhibiti majambazi ipasavyo kwa
kuwanyanganya silaha kwenye matukio ya kiuharifu ili kukomesha vitendo viovu
katika Taifa.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mpango
wa Usalama wa Jamii.
“Inashangaza
jambazi anavamia kituo cha polisi anaua na anaondoka wakati polisi wapo na wana
silaha na risasi wanazo lakini wanashindwa kumnyang’anya silaha,”alishangaa
Rais Magufuli.
Ameongeza
kuwa ujambazi na vitendo vya uharifu nchini inabidi vikomeshwe mara moja ili
watanzania waishi kwa amani na kufanya maendeleo kwani wananchi wanataka
maendeleo.
Akiongelea
kuhusu maslahi na vitendea kazi kwa jeshi la polisi, Rais Magufuli amesema kuwa
serikali yake itafanya kila iwezalo kuliwezesha jeshi hilo ili liweze kufanya
kazi kwa ubora zaidi.
Rais
Magufuli ameonyesha kuwa na imani na jeshi la polisi licha ya kuwa na kasoro
ndogo ndogo kwa baadhi ya polisi ambao wanalichafua jeshi hilo.
Aidha
ametoa agizo kwa TCRA kushirikiana na jeshi la polisi nchini ili kuweza
kurekodi simu na kutoa print out mara
moja tofauti na ilivyo sasa.
Kuhusu
kundi la wafanyakazi wanaofanyakazi kwenye Dawati la Taarifa la polisi, Mhe.
Rais amemtaka Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu kuwafikiria na kuwapatia
posho ya kazi kwani kazi wanayoifanya ni ngumu mno na inahitaji umakini zaidi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemwomba Mhe. Rais
kuliongezea fedha jeshi hilo ili liweze kufanya kazi kwa ustadi zaidi na
kukomesha vitendo vya uharifu nchini.
Makonda
amelipongeza jeshi la polisi kwa kudhibiti matukio ya ujambazi hapa nchini hususan
kwenye mabenki.
Mpango
huu wa Usalama wa Jamii umezinduliwa leo na utadumu hadi 2019 na unatarajiwa
kutoa matokeo makubwa ya kudhibiti uharifu nchini.
No comments:
Post a Comment