TANGAZO


Tuesday, May 3, 2016

Wavalia vyuma katika tamasha la Met


Image captionKatty Perry

Watu maarufu katika tamasha la sanaa ya makavazi mjini New York walivalia mavazi ya vyuma huku wakisheherekea mkutano wa binaadamu na Mashini.

Image captionKarolina Kurkova

Hatahivyo sio wote waliohudhuria tamasha hilo walivaa kulingana na madhari ya tamasha hilo.

Image captionBeyonce Knowles

Tamasha hilo la kila mwaka huiletea mamilioni ya fedha taasisi ya nguo za makavazi.

Image captionEmma Watson

Mwaka uliopita wale waliohudhuria tamasha hilo walitakiwa kuvaa kulingana na mandhari ya ushawishi wa China katika fesheni za kimagharibi na kulikuwa na ufanisi mkubwa.

Image captionTaylor_Swift

Mwaka huu mandhari ya maonyesho hayo ni Manus x Machina: Fesheni katika miaka ya Teknolojia.

Image captionMadonna

Tiketi mwaka huu ziliuzwa kwa dola 30,000 kwa mtu mmoja,lakini licha ya bei hizo za tiketi ni sherehe ambayo ni vigumu kuhudhuria.

Image captionLady Gaga

Faragha ya wageni hulindwa sana,na uchapishaji wa mitandao ya kijamii baada ya kuingia katika zulia jekundu umepigwa marufuku tangu mwaka jana.

Image captionJuno Temple

Mwaka uliopita zaidi ya dola milioni 12 zilichangishwa katika taasisi hiyo ya mavazi ya makavazi.

No comments:

Post a Comment