Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha Dkt. Mohammed Alawi akiongea na baadhi ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
Mwandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Lyndsey Wajert akiwa tayari kufanyiwa vipimo vya malaria na Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha wakati wa ziara ya waandishi wa Habari hao ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi anayefanya kazi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Katy Migiro wa Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara mkoani Arusha kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
Baadhi ya dawa zilizoidhinishwa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutibu ugonjwa wa malaria nchini.
Moja ya mabango yanayosambazwa nchini kuhamasisha wananchi kufanya vipimo dhidi ya ugonjwa wa malaria.
Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa tayari uwanja wa ndege wa Arusha kwa safari ya kuelekea mkoani Tanga.
Eneo la ukingo wa
Bahari ya Hindi mkoani Tanga ambapo karibu na eneo walipofikia waandishi wa
habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara
yao mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.(Picha na Eleuteri
Mangi-MAELEZO, Tanga)
No comments:
Post a Comment