TANGAZO


Thursday, May 12, 2016

Uchafuzi wa hewa unaongezeka duniani

Image copyrightREUTERS
Image captionChina ni miongoni mwa nchi zenye uchafuzi mkubwa wa hewa
Shirika la afya duniani linasema zaidi ya asilimia 80 ya wakaazi wanaoishi mijini wanapumua hewa ya kiwango ha chini. Katika ripoti mpya WHO linasema uchafuzi wa hewa katika miji unaongeza hatari ya mtu kuugua saratani ya mapafu, kuugua pumu na magonjwa mingine na husababisha kufariki zaidi ya watoto milioni tatu kabla ya kutimiza muda wa kuzaliwa.
Mkurugenzi wa shirikahilo kwa afya ya umma, na mazingira, Maria Neira, amesema viwango vya uchafuzi wa mazingira vimeendelea kuongezeka:
"kwa kiwango cha kadri, hali imezidi kuwa mbaya na kuongeza viwangovya hewa kuchafuka kwa 8% ya idadi ya watu wanaoishi mijini ambapo tunakusanya data kuhusu uchafuzi wa hewa- na wanakabiliwana hewa hiyo chafu na kuchangia kuzuka magonjwa ."
Image copyrightAFP
Image captionIndia na China zina kazi kubwa kukabiliana na hewa chafu
Amesema serikali ni lazima zichukuwe hatua kuokoa maisha: "vifo vya watoto wachanga vinatokea kila mwaka na vinatokana na uchafuzi wa hewa na hili bila shaka ni tatizo kubwa mno. Na ndio sababu ni lazima kuwpeo uhamasisho, tuchukue hatua zaidi na ni lazima nchi zichukue hatua ya kukagua hewa ili kupunguza athari mbaya kwa afya ya watu."
Watu wanaoishi vijijini lakini wanafanya kazi mijni wanaathirika vibaya zaidi, New Delhi, Cairo na Dhaka ndio miji inayoongoza inayokabiliwana uchafuzi wa hewa.
Hewa katika mataifa tajiri inaimarika.
Bi Neira anasema India na China zina kazi kubwa: "tunajua kuwa kuna miji kadhaa China na baadhi ya miji India ambayo ipo katika kiwango cha maeneo yalio na uchafuzi mkubwa kupita muongozo uliotolewa na WHO.
Na kwa hivyo nadhani nchi hizi mbili, India na China, zinahitaji kuchukua hatua kubwa kwasababu hali ni mbaya mno hivi sasa kwa raia."

No comments:

Post a Comment