TANGAZO


Thursday, May 12, 2016

Iran na Saudia zavutana kuhusu Hajj

Image copyrightGETTY
Image captionMji mtukufu katika dini ya kiislamu Makka
Iran inasema imeshindwa kufikia makubaliano na Saudi Arabia kuhusu mipango ya raia wake kuweza kwenda Kuhijji Makka mwezi Septemba.
Ni ishara ya hivi karibuni inayodhihirisha jinsi uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulivyo mbaya.
Iran imerusha lawama zote kwa kushindwa kufikia makubaliano na Saudia.
Inasema Saudia ilionyesha ujeuri, na mwenendo usio sawa katika majadiliano.
Ni mazungumzo yaliofanyika katika wakati ambao sio muafaka.
Kuna mzozo mkubwa kati ya mataifa hayo mawili baada ya ibada ya hajj iliofanyika mwaka jana ambapo mamia ya raia wa Iran walifariki katika mkanyagano uliozuka.
Na baadaye uhusiano wote wa kidiplomasia ulivunjwa kutokana na hatua ya Saudi Arabia kumuua kiongozi wa madhehebu ya Shia anayetoka Iran, Nimr al-Nimr.

No comments:

Post a Comment