Wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma nchini wakifuatilia mada.
Mkurugenzi Msaidizi Bi. Veila Shoo akiwasilisha matokeo kuhusu Ufuatiliaji wa Mifumo na Viwango vya utendaji kazi kwa Taasisi za Umma nchini.Wanaomsikiliza ni sehemu ya wawakilishi kutoka katika Taasisi za Umma.
Na Happy Shayo, Utumishi
TAASISI za Umma zimehimizwa kutumia ipasavyo mifumo ya
utendaji kazi iliyowekwa ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Bi. Veila Shoo alisema hayo wakati akitoa takwimu za matumizi ya mifumo
hiyo katika kikao kazi kilichohusisha wawakilishi kutoka katika Wizara, Idara
Zinazojitegemea na Wakala za Serikali na kufanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
Bi. Veila alieleza kuwa ufuatiliaji wa mifumo umefanyika katika
Idara Zinazojitegemea 16 ambapo imebainika baadhi ya mifumo inatukima ipasavyo
wakati mingine bado.
Awali, akifungua kikao kazi hicho Mkurugenzi wa Idara ya
Uchambuzi na Ushauri Kazi Bw. Mick Kiliba alisema kuwa zoezi la kufanya
ufuatiliaji wa mifumo ni endelevu na watendaji wanatakiwa kuhakikisha
wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kutumia mifumo hiyo.
Alisema lengo la tathmini hiyo ni kupata takwimu za
utekelezaji wa mifumo na viwango vya utendaji kazi, kutambua mifumo yenye
changamoto za utekelezaji, kutoa hamasa ili kuboresha utoaji huduma na kutoa
mrejesho kwa taasisi jinsi ya kuimarisha mifumo.
Mifumo iliyofanyiwa tathmini ni pamoja na:- Mpango mkakati Mkataba
wa Huduma kwa Mteja; Mfumo wa wazi wa Tathmini ya Utendaji kazi; Uboreshaji wa
michakato ya Utoaji huduma; Tathmini ya Utoaji huduma wa Taasisi; Tathmini ya
ndani ya Taasisi; Ushirikiano wa Taasisi ya Umma na Asasi za Kiraia(AZAKI); Waraka
Namba 1 wa mwaka 2012 kuhusu Ununuzi wa Samani za Ofisi; na Usimamizi wa Fomu za Serikali.
No comments:
Post a Comment