Na Benedict Liwenga, Maelezo, Dodoma.
SERIKALI imepiga marufuku upakiaji wa mizigo kupita kiasi (lumbesa) katika magunia kuanzia mwaka ujao wa fedha.
Kauli hiyo imetolewa jana Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) wakati akijibu hoja mbalimbali za Wabunge wakiochangia hotuba ya Wizara yake.
Amesema kuwa, kuanzia mwaka ujao wa fedha, Vyombo vy Dola vitakamata wafanyabiashara wote watakaokuwa wanapakia lumbesa.
Mhe. Mwijage alisema kuwam upakiaji huo wa mizigi kupita kiasi unawasababishia wizi kwa wakulima ambapo ametoa wito kwa wakulima na wafanyabiashara nchini kutumia vipimo halali wakati wanaponunua na kuuza mazao yao mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo ametoa wito kwa wakulima kuacha tabia ya kuuza mazao yao yakiwa shambani au kabla ya kukomaa.
Alisema kuwa hali hiyo inawarudisha nyuma na kuwapunja wakati wangesubiri mazao yakomae wangepata fedha za kutosha.
No comments:
Post a Comment