Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mbarak Abdulwakil (kushoto) akifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ngosi Mwihava.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO.
SERIKALI imeandaa
mkakati mpya wa kitaifa wa kupanda na kutunza miti ili kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi hatua ambayo itarudisha hali ya mazingira kama
yalivyokuwa awali miaka ya nyuma.
Hayo yamesemwa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba
alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo
hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.
“Mkakati huu mpya umezingatia kurekebisha changamoto
zilizojitokeza katika kampeni za upandaji miti zilizofanyika katika vipindi
mbalimbali tangu uhuru wan chi yetu” alisema Waziri Makamba.
Ili kukabiliana na
changamoto hizo, Waziri Makamba amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake
imetenga kiasi cha Sh. bilioni 2 ikiwa kianzio kwa lengo la kusimamia mkakati
huo katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Katika kuhakikisha
suala la mazingira limepewa kipaumbele, Mfuko wa Taifa wa Mazingira ambao ni
mdau mkuu wa mazingira utatengewa vyanzo vya mapato yanayokadiriwa kufikia Sh.
bilioni 100 ikiwa ni juhudi za kugharimia mpango huo na mipango mingine ya
hifadhi ya mazingira.
Mkakati huo ni wa
miaka mitano ambao unaanza kutekelezwa 2016 hadi 2021 na unakadiriwa kugharimu
kiasi cha Sh. bilioni 105.2.
Aidha, Waziri Makamba
amebainisha kuwa masuala ambayo yatazingatiwa katika kutekeleza mpango huo ni
pamoja na uhamasishaji na utoaji motisha kwa watumiaji wa nishati mbadala ili
kuondoa matumizi ya kuni na mkaa.
Ili kuhakikisha
mazingira yameboreshwa na yawe rafiki kwa kila kiumbe, utekelezaji na
usimamiaji wa mkakati huo, utaanza kutekelezwa kuanzia ngazi ya chini hadi juu
ambapo kila kijiji, kitongoji, mtaa, kaya na kila taasisi itapewa lengo la
pandaji miti kama msingi wa zoezi hilo.
“Tutashindanisha
shule na vijiji katika upandaji na ukuzaji wa miti na tutatoa zawadi nono na
maeneo ya wazi ya Serikali yatapandwa miti” alisema Waziri Makamba.
Katika kuhakikisha
miti iliyopandwa inalindwa na kukua, Ofisi
ya Makamu wa Rais itashirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mkioa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha halmashauri zinatunga sheria ndogo ndogo za
kuhimiza upandaji na utunzaji miti nchini.
Maadhimisho ya mwaka
huu Kimataifa yanafanyika nchini Angola ambayo yanalenga kupambana na biashara
ya meno ya tembo na pembe za faru yakiongozwa na kaulimbiu “Tunza wanyama porini
kwa maisha”.
Siku ya mazingira
Duniani imeanza kuadhimishwa mwaka 1972
ambapo Baraza la Umoja wa Mataifa lilifanya wa mkutano wake wa kwanza unaohusu
mazingira uliofanyika Stockholm nchini Sweden na kuundwa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia mazingira diniani (UNEP).





No comments:
Post a Comment