Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akisaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo nchini ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akiongea na wadau wa maendeleo mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wake wa Kunusuru Kaya Masikini nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird.
Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird jijini Dar es slaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wiazara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Wadau wa Maendeleo wakimskiliza Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird wakati wa mkutano jijini Dar es Salaam.
Baaadhi ya waandishi wa habari (waliosimama) wakiendelea na kazi yao wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo nchini ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini. Kaimu Mkurugenzi Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Daniel Moore (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wiazara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kulia) mara baada ya hafla ya kusaini mkataba na wadau wa maendeleo jijini Dar es salaam ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Maendeleo nchini. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga (wa kwanza kulia).
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO,Dar es Salaam
SERIKALI ya Tanzania
imesaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 na
Wadau wa Maendeleo ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika
Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.
Mkataba huo ambao umetiwa
saini jijini Dar es Salaam unawataka watendaji kuweka utaratibu ambao unaenda
sambamba na Mpango wa utekelezaji bila kuingilia majukumu ya mamlaka ya Serikali
katika utekelezaji wa TASAF wa kunusuru kaya masikini.
Akizungumzia mkatraba
huo mara baada ya kusaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Katibu Mkuu Wiazara
ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa mpango huo
unaosimamiwa na TASAF unalenga kuziwezesha kaya masikini nchini kujiongezea
kipato na kupata chakula cha kutosha pamoja na kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Katika kutekeleza
mpango huo wa TASAF uwe wa tija kwa kaya masikini kulingana na malengo
tarajiwa, mpango umegawanyika katika maeneo makuu manne ambayo yanatarajiwa
kuboresha hali za watu wanaoishi katika hali duni nchini.
Maeneo hayo yanayotekelezwa
ni pamoja na kuhawilisha fedha kwa kaya masikini hasa zile zenye watoto ili
ziweze kupata huduma za elimu kwa kuwawezesha watoto walio katika shule za
msingi na sekondari kupata mahitaji muhimu shuleni pamoja na kupata huduma za
afya na kuongeza kipato kwa kaya masikini kupitia uwekaji akiba na shughuli za
kiuchumi.
Maeneo mengine ya
utekelezaji huo ni kutoa ajira ya muda kwa kaya masikini zenye watu wenye uwezo
wa kufanya kazi wakati wa kipindi cha njaa na majanga yakiwemo ukame na
mafuriko pamoja na kujenga uwezo katika ngazi zote za uteklelezaji wa kutoa
mafunzo yatakayoboresha utekelezaji wake.
Mpango wa Kunusuru
Kaya Masikini nchini umekuwa na
mafanikio nchini ambapo hadi sasa umeshahawilisha kwa walengwa mizunguko 14 ya
malipo ya jumla ya fedha zote
zilizohawilishwa kufikia bilioni Sh. 224 na kuandikisha kaya milioni 1.1
tangu uanzishwe mwaka 2012 na kuhudumia halmashauri
159 Tanzania Bara pamoja na halmashauri 11 Tanzania Zanzibar.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Wadau hao wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa
Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi.
Bella Bird amesema kuwa makubaliano yaliyotiwa saini yataboresha uhusiano na
kuendeleza majadiliano baina ya Serikali na wadau kuhusu kunusuru kaya masikini
na kutoa msaada wa kitaalamu utakaohitajika ili kufikia malengo yanayotarajiwa.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga amewahakikishia
wadau hao wa maendeleo kuwa fedha walizotoa kwa mfuko huo zitatumika kwa
malengo yaliyowekwa ili kuwasaidia Watanzania wanaoishi katika hali duni waweze
kuinua hali zao kiuchumi na kupata mahiji yao ya kila siku.
Wadau waliotia saini
mkataba huo wa makubaliano ya kunusuru kaya masikini ni pamoja Benki ya Dunia,
Ubalozi wa Sweden, Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Mpango wa
Maendeleo wa Umoja wa Mtaifa (UNDP), Shirika la Misaada la Marekani (USAID),
Shirika la Watoto la Umojas wa Mtaifa (UNICEF), Shirika la Kazi Duniani (ILO)
na Shirika la Watu wa Umoja wa Mataifa (UNFPA), Wizara ya Fedha na Mipango na
TASAF kwa upande wa Tanzania.










No comments:
Post a Comment