TANGAZO


Wednesday, March 16, 2016

Simbachawene awataka Ma-RC wafanye kazi kulingana na kasi ya Rais Magufuli

Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa kutoka TAMISEMI Bi. Suzani Chekani akionesha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwasilisha mada kuhusu kuwajibika kwa kuzingatia sheria za nchi kwa wakuu wa mikoa wapya katika kikao kilichofika leo Jijini Dar es Salaam  kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene. (Picha zote na Raymond Mushumbusi - MAELEZO)
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Suleiman Jafo, akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa wizara hiyo, George Simbachawene (kushoto), kuzungumza na Wakuu wa Mikoa (hawapo pichani), akiwataka kwenda kuwajibika kwa kuzingatia sheria na kutatua changamoto za wananchi katika Mikoa yao katika kikao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wakuu wa mikoa (hawapo pichani) akiwataka kwenda kuwajibika kwa kuzingatia sheria na kutatua changamoto za wananchi katika mikoa yao katika kikao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia maelekezo toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) katika kikao cha kuwakumbusha majukumu yao kama wakuu wa mikoa. 
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia maelekezo toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) katika kikao cha kuwakumbusha majukumu yao kama wakuu wa mikoa. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mhe. George Simbachawene (kutoka wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa mikoa wapya walioapishwa jana kulia mwa Waziri ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo. 

Na Jacquiline Mrisho Maelezo
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI, Mhe.George Simbachawene amewataka Wakuu wa Mikoa walioapishwa kufanya kazi kwa bidii na kutumia muda mwingi kutatua kero zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.

Mhe.Simbachawene ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam alipokutana na Wakuu hao wa Mikoa ambapo amewasisitiza kwenda na kasi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kutimiza malengo yaliyopangwa katika uongozi wa Serikali ya awamu ya tano.

“Mfumo wa sasa wa uongozi ni tofauti na mfumo wa zamani, namna Mhe. Rais anavyotaka tufanye kazi ni tofauti na zama zingine zilizopita,Wakuu wa Mikoa mnapaswa kujua kila kinachoendelea kila siku katika Mikoa yenu na mnapaswa muwajibike kwa wananchi wenu”alisema Simbachawene.

Mhe.Simbachawene ameongeza kuwa,Wakuu wa Mikoa wamepewa madaraka ya kusimamia mfumo wa ufanyaji kazi kwa kuhakikisha watumishi wa umma  wanawajibika ipasavyo kwakua nchi haiwezi kubadilika kama hakutakua na utendaji mzuri.

Aidha,Mhe.Simbachawene amewakumbusha Wakuu wa Mikoa wazingatie na kusimamia haki za wananchi kwakua kuna baadhi ya mamlaka za Serikali za Mitaa zinaripotiwa kuwaonea sana wananchi hasa wanawake katika kupata haki zao maana ndio wanaongoza kwa kunyanyaswa.

Pia amewataka Wakuu wa Mikoa kutumia mamlaka waliyopewa kuvunja mabaraza yote ya usuluhishi yasiyozingatia sheria katika kutoa maamuzi na kuunda mabaraza mapya yenye sifa za kutatua kesi za wananchi.

Naye Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI, Mhe. Selemani Jaffo ameahidi kuwapa Wakuu wa Mikoa ushirikiano wa kutosha kutoka Ofisi ya TAMISEMI ili kuhakikisha kazi zao  zinafanyika kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment