TANGAZO


Sunday, March 20, 2016

Salah kushtaki mwendesha mashtaka

Image copyrightAP
Image captionSalah Abdeslam akikamatwa nchini Ubelgiji
Wakili wa mshukiwa wa shambulizi la Paris Salah Abdeslam anasema kuwa atamchukulia hatua za kisheria mwendesha mashtaka nchini ufaransa kwa kufichua siri ya mshukiwa.
Mwendesha mashtaka huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa Abdeslam alikiri kuwa alikuwa na mipango ya kujilipua wakati wa mashambulizi ya mwezi Novemba lakini baadaye akabadili mawazo yake.
Milipuko na ufyatuaji risasi ambavyo vinadaiwa kufanywa na kundi la Islamic state, ilisababisha vifo vya watu 130 ambapo pia wengine kadha walijeruhiwa.
Abdeslam alikamatwa nchini Ubelgiji wiki iliyopita miezi minne baada ya kuwa mafichoni.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Paris siku ya Jumamosi, mwendesha mashtaka wa mjini Paris Francois Molins, akinukuu taarifa ya polisi wa Ubegiji akisema kuwa mshukiwa alitaka kujilipua katika uwanja wa State de France.

No comments:

Post a Comment