Msajili wa Vyama vya Siasa
akizungumza na mmoja wa wasimamizi wa Uchaguzi wa marudio mara
baada ya kufika katika kituo cha kupiga kura cha Nungwi kilichopo Unguja
Zanzibar katika uchaguzi wa marudio uliofanyika leo.
Na Monica Laurent, Zanzibar.
WAKAZI
wa Unguja na Pemba wametakiwa kuienzi Amani
iliyopo Visiwani Zanzibar kwa kuachana na kufanya vitendo vinavyoweza kuleta uvunjifu
wa Amani visiwani humu.
Rai
hiyo imetolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi ambaye
yuko visiwani humu akiwa na timu wa watu wanne kutoka ofisi yake kwa ajili ya uangalizi wa uchaguzi wa marudio
uliofanyika leo hii . Aliyasema hayo alipohojiwa na Mtangazaji wa kituo cha
Radio cha Zenji Fm Bw.Jumanne Ramadhani mara baada ya kufanya uangalizi katika
kituo cha kupiga kura cha Nungwi kilichopo Unguja Zanzibar. Ofisi ya Msajili ni
miongoni mwa waangalizi wa ndani wa Uchaguzi waliofika Zanzibar kwa ajili ya
uangalizi wa uchaguzi.
Aidha
Jaji Mutungi ametoa rai kwa vyombo vya habari kuhakikisha vinalipoti masuala ya
uchaguzi kwa ueledi ili visije vikawa chanzo cha uchochezi kwa jamii jambo
ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment