TANGAZO


Wednesday, March 23, 2016

MKUU WA MKOA WA PWANI ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA BAGAMOYO

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo akimjulia hali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Ibrahim Matovu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) anapo endelea kupatiwa huduma mapema  Dar es Salaam leo, ambapo anatarajiwa kuruhusiwa kwa leo au kesho kutokana na haliyake kuendelea vizuri (Picha zote na Khamisi Mussa)
Diwani wa Kata ya Kilomo, Bagamoyo, Hassan Usinga (Wembe) akimjulia hali Afisa Maendeleo ya Jamii ya Bagamoyo Julius Mwanganda mara alipofika katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) anapopatiwa matibabu kutokana na ajali mbaya iliyotokea mkoani  humo hivi karibuni.
Diwani wa Kata ya Maboga iliyopo wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, Vemi Chambala akimsimulia   Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo (aliyefunga mikono) wakati alipofika katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)  Muhimbili, kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Bagamoyo  ambapo wanapata matibabu kutokana na ajali mbaya iliyotokea mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo, akimjulia hali Ofisa Maendeleo ya Jamii ya Bagamoyo Julius Mwanganda.

No comments:

Post a Comment