Manchester United walichapwa 2-0 mechi ya mkondo wa kwanza
Mechi za marudiano za raundi ya mtoano ya timu 16 za Uefa Europa League zitaendelea leo Alhamisi kwa michezo minane.
Tottenham, maarufu kama Spurs wako kwao White Hart Lane Jijini London kurudiana na Vigogo wa Germany Borussia Dortmund ambao walishinda Mechi ya kwanza 3-0 na hivyo Spurs wanapaswa kushinda 4-0 ili kusonga.Nako huko Old Trafford ni marudiano ya mahasimu wakubwa wa Soka la England ambapo Man United wanatakiwa waifunge Liverpool 3-0 ili wasonge baada ya kutandikwa 2-0 Wiki iliyopita huko Anfield kwa Bao za Penati ya Daniel Sturridge na Roberto Firmino.
- Manchester United 23:05 Liverpool
- Tottenham Spurs 23:05 Borusia Dortmund
- Bayer Leverkusen 21:00 Villarreal
- Lazio 21:00 Sparta Prague
- Valencia 21:00 Athletico Bilbao
- Anderlecht 23:05 Shaktar Donetsk
- Sevilla 23:05 FC Basel
- Sporting Braga 23:05 Fenerbahçe

No comments:
Post a Comment