Taifa la Korea Kaskazini limerusha makombora kadhaa ya masafa mafupi katika maji ya pwani yake ya mashariki ,kulingana na kituo cha habari cha Korea Kusini Yonhap.
Washington na Seoul zinafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi huku Korea Kaskazini ikidhania inajiandaa kuivamia.Vikwazo vipya dhidi ya taifa hilo vinatokana na hatua ya taifa hilo kuyafanyia majaribio makombora yake ya kinyuklia pamoja na uzinduzi wa kifaa chake cha Satelite mnamo tarehe 7 mwezi Februari ambayo ilikiuka vikwazo vya Umoja wa mataifa vilivyopo.
Korea Kusini ilikuwa ikijaribu kubaini ni aina gani ya makombora yaliohusishwa katika urushaji huo.
Makombora hayo yalidaiwa kurushwa kutoka mji wa Kaskazini Mashariki wa Hamhung.
Siku ya ijumaa Korea Kaskazini ilirusha makombora mawili ya masafa marefu.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa makombora hayo yaliruka kilomita 800 kabla ya kuanguka majini.
Baadaye Marekani iliitaka Pyongyang kutosababisha wasiwasi.
No comments:
Post a Comment