Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu, Damian Lubuva
Na Jacquiline Mrisho –MAELEZO
Na Jacquiline Mrisho –MAELEZO
Dar es Salaam 24.03.2016
MWENYEKITI
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu, Mhe. Damian Lubuva amekamilisha uchaguzi wa mwaka 2015 baada ya
kumaliza kuteua wabunge wanawake watatu wa viti maalumu waliokuwa wamebakia.
Uteuzi
huo umefanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kutangazwa rasmi leo Jijini
Dar es salaam na Jaji Mstaafu Lubuva kwenye mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za tume hiyo.
“Tume
ya Taifa ya Uchaguzi imewateua ndugu Ritah Kabati na Oliver Semuguruka wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) na Lucy Owenya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kuwa wabunge wanawake wa viti maalum katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.”alisema
Lubuva.
Jaji
Mstaafu Mhe. Libuva ameongeza kuwa,kwa mwaka 2015 NEC ilitakiwa kuteua wabunge wanawake
wa viti maalum 113 ila waliteuliwa jumla ya wabunge 110 ambapo viti vitatu
vilibakia kusubiri uchaguzi wa majimbo 8 ambayo uchaguzi wake ulihairishwa
kutokana na sababu mbalimbali.
Jaji
Mstaafu Lubuva amesema kuwa,NEC hufanya uteuzi wa wabunge wanawake wa viti
maalum kutoka kwenye orodha iliyotumwa na Katibu Mkuu wa chama husika hivyo,
Tume imewateua wabunge hao kama walivyoorodheshwa kwenye majina yaliyoletwa na
makatibu wao.
Hatimaye
zoezi la uchaguzi wa mwaka 2015 kwa sehemu zilizosalia limeisha kwa amani, viongozi waliochaguliwa na
kuteuliwa wana wajibu wa kufanya kazi yakuwatumikia wananchi ili kuleta
maendeleo kwa Taifa.
No comments:
Post a Comment