Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) akuzungumza katika Mkutano Mkuu Muhula wa Kwanza wa mwaka 2016 wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Mwanza uliofanyika Jumamosi Machi 19,2016 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Pamba Jijini Mwanza. Kushoto kwake ni viongozi wa bodaboda Mkoa wa Mwanza.
Katika Mkutano huo, Konisaga ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alitaka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabara kuzidisha juhudi za kutoa elimu ya usalama barabarani ili kupunguza ajali, badala ya kasi iliyopo ya kutoza faini kwa watumiaji wa vyombo vya barabarani.
Mwenyekiti wa bodaboda Mkoa wa Mwanza Makoye Kayanda amesema "pamoja na Mambo mengine, Wajumbe wa Mkutano huo walikubaliana kwa sauti moja kuanzishwa kwa Umoja wa Bodaboda Taifa ili kurahisisha utatuzi wa Changamoto zinazoikabiri sekta ya usafirishaji abiria ya Bodaboda".
Kwa Habari Zaidi BONYEZA HAPA.
No comments:
Post a Comment