Balozi Seif akionyesha hati yake aliyokabidhiwa mara baada ya kushinda uchaguzi Jimbo la Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unaguja.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Makame Pandu Khamis akimkabidhi hati ya Ushindi Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Kiwengwa Bibi Asha Abdulla Mussa hapo Skuli ya Sekondari ya Mahonda.
Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Bumbwini Bibi Mtumwa Pea Yussuf akionyesha kwa furaha Hati yake iliyomthibitisha kuwa ameshinda Uchaguzi katika Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
21/3/2016.
SHAMRA shamra za kusherehekea ushindi kufuatia
kukamilika kwa Uchaguzi wa Marejeo uliokipa nafasi Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kuendelea kuongoza Dola zimeanza katika maeneo mbali mbali Mjini na Vijijini
Unguja na Pemba.
Furaha hizo zilianza mara baada ya Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Zanzibar Nd. Jecha Salum Jecha kutangaza washindi kwenye
kinyang’anyiro hicho hapo katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini
Zanzibar jana.
Sherehe hizo zilikwenda sambamba na wawakilishi
pamoja na madiwani wateule kwenye majimbo na wadi kukabidhiwa vyeti vyao vya
ushindi na maafisa wa Tume ya Uchaguzi wa Wilaya.
Msimamizi
wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu
Makame Pandu Khamis alikabidhi vyeti kwa washindi wateule wa Majimbo na
Wadi zilizomo ndani ya Wilaya ya hiyo hafla hiliyofanyika
katika uwanja wa Skuli ya Sekondari ya Mahonda Mkoa wa Kaskazini
Unaguja.
Waliokabidhiwa vyeti hivyo ni Mwakilishi Mteule wa
Jimbo la Mahonda ambaye pia ni makamu wa Pili wa Raisw wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi, Bibi Asha Abdulla Muusa Mwakilishi mteule wa Jimbo la Kiwengwa pamoja
na Mwakilishi mteule wa Jimbo la Bumbwini Bibi Mtumwa Pea Yussuf.
Dr. Khalid Salum Mohammed ni Mwakilishi Mteule wa wa Jimbo la Donge
ambae alidharurika katika hafla hiyo fupi.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya Wawakilishi na Madiwani
wateule wa Majimbo na Wadi zilizomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”
wakati wa
kusherehekea ushindi huo hapo Ofisi ya CCM Wilaya iliyopo Mahonda
Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi
aliwashukuru Wanachama
na Wananchi wa Majimbo ya Wilaya hiyo kwa umakini wao wa kuirejesha tena
madarakani CCM.
Balozi Seif pia aliwashukuru wasimamizi wa Tume ya
Uchaguzi pamoja na Mawakala wa vyama vya Siasa kwa kazi kubwa waliyoifanya
iliyosaidia kuendeshwa kwa uchaguzi huo wa marejeo kwa amani na usalama.
Balozi Seif alisema jukumu walilobeba wasimamizi na
mawakala hao limewawezesha wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi kupata
haki zao katika uchaguzi huo kwa mujibu wa jinsi walivyonadi sera zao.
Wawakilishi na Madiwani hao wateule wa majimbo ya
Wilaya ya Kaskazini “B” wameahidi kuwatumikia vyema wananchi wao katika kipindi
cha miaka mitano ijayo.
BaloziSeif aliwahakikishia wananchi wa Majimbo hayo
kwamba kazi rasmi ya kuwatumikia inatarajiwa kuanza rasmi muda mfupi ujao mara
baada ya kukamilika kwa taratibu wa kisheria.
Mwakilshi mteule huyo wa Jimbo la Mahonda waliwataka
wanachama wa chama cha Mapinduzi kuwa waangalifu na kuchukuwa tahadhari wakati
wote wa kusherehekea ushindi wao.
No comments:
Post a Comment