TANGAZO


Thursday, March 17, 2016

AU kutuma waangalizi wa uchaguzi Zanzibar

Matokeo  
Matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana yalifutwa
Tume ya Umoja wa Afrika imetangaza kwamba itawatuma waangalizi wa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar ambao utafanyika Jumapili.
Vyama sita vya upinzani, kikiwemo Chama cha Wananchi (CUF) vimetangaza kwamba vitasusia uchaguzi huo.
Uchaguzi huo unatokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais na wawakilishi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana.
Chama cha CUF kilipinga hatua ya kufutwa kwa matokeo hayo.
Mgombea wake wa urais, Maalim Seif Sharif Hamad, alijitangaza mshindi wa uchaguzi huo wa mwaka jana.
Juhudi za kutumia mazungumzo kutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa uliotokana na kufutwa kwa matokeo hayo hazikufua dafu.
Kupitia taarifa, AU imesema: “Kuambatana na wajibu wake, Tume ya Umoja wa Ulaya itatuma ujumbe wa wataalamu Zanzibar kuhakikisha kwamba uchaguzi wa marudio ni wa amani, wa kuaminika na unatimiza viwango vya AU vya uchaguzi wa kidemokrasia.”
Ujumbe huo utakuwa visiwani Zanzibar kati ya tarehe 17 na 25 Machi.

No comments:

Post a Comment