TANGAZO


Friday, March 25, 2016

Adam Johnson afungwa jela miaka sita

Johnson Johnson alikuwa amechezea England mara 12

Mchezaji soka Adam Johnson amefungwa jela miaka sita kwa kushiriki mapenzi na msichana wa miaka 15.
Jaji amemwambia Johnson, 28, kwamba alihsiriki ngono na msichana huyo akifahamu vyema kwamba alikuwa na umri wa chini ya miaka 16.
Imebainika pia kwamba polisi walipata kanda chafu za video zinazohusisha wanyama kwenye kompyuta mpakato ya Johnson.
Hata hivyo, hatachukuliwa hatua kutokana na hilo.
Johnson
Mahakama ya Bradford iliambiwa kwamba mchezaji huyo alishiriki mapenzi na msichana huyo katika gari lake aina ya Range Rover Januari 2015.
Johnson alichezea timu ya taifa ya England mara 12. Alikuwa mchezaji wa klabu ya Sunderland.

No comments:

Post a Comment