Meneja Uhusiano wa Kampuni ya ving'amuzi ya StarTimes, Muddy Kimwery akibofya kitufe cha kompyuta kuchezesha droo ya nne ya Pasua Anga kwa ajili ya kumpata mshindi wa nne kati ya washindi 5 watakaokwenda Ujerumani kuangalia Ligi Kuu ya nchi hiyo, Bundesliga, jijini Dar es Salaam jana. Kulia anayeangalia ni Mkaguzi wa michezo ya Kubahatisha nchini, Bakari Maggid.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya ving'amuzi ya StarTimes, Muddy Kimwery akibofya kitufe cha kompyuta kuchezesha droo ya nne ya Pasua Anga kwa ajili ya kumpata mshindi wa nne kati ya washindi 5 watakaokwenda Ujerumani kuangalia Ligi Kuu ya nchi hiyo, Bundesliga, jijini Dar es Salaam jana. Kulia anayeangalia ni Mkaguzi wa michezo ya Kubahatisha nchini, Bakari Maggid.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya ving'amuzi ya StarTimes, Muddy Kimwery akimuonesha namba ya mshindi Mkaguzi wa michezo ya Kubahatisha nchini, Bakari Maggid wakati wa kuchezesha droo ya nne ya Pasua Anga kwa ajili ya kumpata mshindi wa nne kati ya washindi 5 watakaokwenda Ujerumani kuangalia Ligi Kuu ya nchi hiyo, Bundesliga, jijini Dar es Salaam jana.
Mfanyakazi wa Kituo cha Mawasiliano cha Kampuni ya ving'amuzi ya StarTimes, Rehema Luponda akiwasiliana na mshindi wa nne wa droo ya nne wa Pasua Anga, Joseph Mogela (46), mkazi wa Kibamba jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuchezeshwa droo hiyo, jijini jana. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Muddy Kimwery na katikati ni Mkaguzi wa michezo ya Kubahatisha nchini, Bakari Maggid.
Dar es Salaam, Februari 26, 2016
IKIWA imebakia droo moja ya bahati
nasibu ya kujishindia safari ya kwenda Ujerumani inayoendeshwa na kampuni ya
StarTimes Tanzania, mkazi wa Kibamba, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw.
Joseph Mogela (46) ambaye ni dereva katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili amebahatika kuwa mshindi wa nne wa safari hiyo ya
kusisimua.
Akizungumza kwa njia ya simu Bw.
Mogela alielezea kuwa amefurahi sana kwa kutangazwa huko hasa ukizingatia
promosheni hiyo inaelekea ukingoni.
“Nimefurahi sana na nawashukuru
StarTimes kwa kunitangaza mimi kuwa mshindi wa droo ya nne ya promosheni hii.
Sikutegemea kwa kweli kwa sababu mimi nililipitia kama mteja mwingine ambaye
anafurahia huduma za kampuni hii. Lakini nimeshtushwa na simu hii kuwa mimi
ndiye mshindi wa droo hii kubwa ambayo ni fursa kubwa sana kwangu mimi.” Alisema
Bw. Mogela
“Nashukuru kwa nafasi hii
niliyopatiwa ambayo naweza kusema imepatikana kwa mtaji wa kulipia kifurushi
cha Mambo kinachopatikana katika king’amuzi cha StarTimes kwa shilingi 12, 000/
tu kwa mwezi. Wakati mwingine sisi wateja huwa tunadharau vitu hivi lakini
vinakuwa ni vya kweli, ninaamini mpaka napigiwa simu hii na kuipokea basi
bahati ilikuwa ni ya kwangu,” alisema na kumalizia mshindi huyo, “Ningependa
kushukuru tena na ninaisubiria hiyo safari kwa hamu kwani kupata fursa ya
kwenda Ujerumani kutazama mechi ‘Laivu’ tena bila ya gharama si mchezo. Nawasihi
wengine wasipitwe na promosheni hii.”
Naye kwa upande wake Meneja
Uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Muddy Kimwery amebainisha kuwa sasa mambo
yanakaribia kuiva kwani huyo alipatikana alikuwa ni mshindi wa nne maana yake
kwamba amebakia mmoja tu kutangazwa ili kukamilisha idadi ya watano kama
tulivyoahidi.
“Leo tumechezesha droo ya nne kwa
wateja wetu kujishindia safari ya kwenda Ujerumani kushuhudia mechi ya
Bundesliga moja kwa moja uwanjani. Mshindi wetu wa leo anatokea hapahapa Dar es
Salaam, anaitwa Joseph Mogela ana umri wa miaka 46 na anafanya kazi ya udereva
pale Muhimbili katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi. Mshindi huyu
anaungana na wengine watatu na amebakia mmoja ambaye tunatarajia wiki ijayo
tutampata ili aweze kujumuika na wenzake tayari kwa safari ya pamoja.” Aliongezea
Bw. Kimwery
Meneja huyo wa Uhusiano wa Umma
kutoka StarTimes alimalizia kwa kusema kuwa, “Najua washindi wetu
waliokwishapatikana wana shauku kubwa ya kutaka kujua ni mechi gani
watakayoenda kuangalia, lini wataondoka na kurudi. Ningependa kuwatoa hofu,
mipango yote inaendelea na tutawafahamisha wote kila kitu kupitia vyombo vya
habari kama tulivyofanya kwa kuwaatangaza washindi. Ningependa kuwaambia
wajiandae kwani mambo yameanza kuiva, safari inanukia na natoa wito kwa wateja
wengine waendelee kulipia na kujiunga na huduma Zetu kwani bado nafasi ni kubwa
ya kubahatika na safari hii ya kipekee.”

No comments:
Post a Comment