TANGAZO


Friday, February 5, 2016

Kambi ya Upinzani yatangaza Mawaziri wake

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe

Na Raymomd Mushumbusi-Dodoma)
KIONGOZI wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni  Mhe Freeman Mbowe Mbunge wa Hai (Chadema) ametangaza rasmi Baraza la Mawaziri vivuli litakalosaidiana na Serikali katika kuendesha shughuli za kimaendeleo.

Akitangaza Mawaziri hao vivuli  kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani amesema anawaomba Mawaziri wa Wizara husika kuwapa ushirikiano wale wote walioteuliwa kuwa Mawaziri vivuli katika Kambi ya Upinzani  ili kupeleka mbele gurudumu la maendeleo nchini.

Waliotangazwa katika orodha hiyo, ni pamoja na Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora,Jaffar Michael, Manaibu wake ni Joseph Nkundi na Ruth Mollel, Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Ali Saleh Abdalla na Naibu wake ni Pauline Gekul, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Esther Bulaya na Manaibu ni Yusuph Makame na Maftah Abdalla, Wizari wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ina Mawaziri wawili ambao ni Magdalena Sakaaya na Emmaculate Swari, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Inj. James Mbatia na Naibu Waziri ni Willy Kombucha.

Aidha, ameendelea kuwataja Mawaziri wengine kuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango, Halima Mdee  na Naibu Waziri ni David Silinde, Waziri wa Nishati na Madini John Mnyika na Naibu Waziri ni John Heche Waziri wa Katiba na Sheria ni Tundu Lissu na Naibu Waziri ni Abdalla Mtolela, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ni Peter Msigwa na Naibu Waziri ni Riziki Shaghali, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ni Juma Omari na Naibu Waziri ni Mwita Waitara, Waziri ya Mambo ya Ndani ni Godbless Lema  na Naibu Waziri Masoud Abdalla, Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni Wilfred Lwakatare na Naibu waziri ni Salum Mgoso. 

Wengine walioteuliwa katika Baraza kivuli ni Waziri wa Maliasili na Utalii Esther Matiko na Naibu ni Waziri Cecilia ParesoWaziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ni Anthony Komu na Naibu Waziri ni Cecil Mwambe, Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi ni Suzan Lyimo, Naibu Waziri ni Dkt. Ali Suleiman Yusuph, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni Dkt. Godwin Mollel na Naibu Waziri Zubeda Sakul, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ni Joseph Mbilinyi na Naibu Waziri  ni Devotha Minja na Waziri wa Maji na Umwagiliaji ni Hamidu Hassan na Naibu Waziri ni Peter Lijualikali.

No comments:

Post a Comment