TANGAZO


Friday, January 1, 2016

Welbeck awatakia heri mashabiki wa Arsenal Kenya

Welbeck

Image copyrightPA
Image captionWelbeck hajachezea Arsenal tangu aumie mwezi Aprili
Mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck amewatumia salamu za heri ya mwaka mpya mashabiki wa Arsenal walio Kenya kwa niaba ya klabu hiyo.
Mchezaji huyo aliyetoka Manchester United mwaka 2014 ametuma ujumbe huo kupitia video ambayo imepakiwa kwenye ukurasa wa Facebook wa klabu ya Arsenal.
Klabu hiyo imepakia video nyingine ya meneja Arsene Wenger akiwatakia heri mashabiki wa klabu hiyo duniani.
"Heri ya Mwaka Mpya Kenya kutoka kwa kila mtu hapa Arsenal,” anasemaWelbeck kwenye video hiyo.
Baadaye, kumeandikwa ujumbe kwa Kiswahili "Heri ya Mwaka Mpya 2016”.
Ujumbe huo wa Arsenal umetolewa siku chache baada ya Arsenal kulazwa 4-0 na Southampton, ambao walisaidiwa sana na Mkenya Victor Wanyama.
WelbeckImage copyrightEPA
Image captionWelbeck akichezea Arsenal dhidi ya Manchester United Machi mwaka jana
Welbeck, aliyewafungia Gunners mabao manane kutoka kwa mechi alizowachezea, hajacheza kwa miezi kadha baada ya kuumia goti wa mechi ya nyumbani dhidi ya Chelsea mwezi Aprili mwaka uliopita.
Mechi hiyo iliisha sare tasa.
Welbeck alifanyiwa upasuaji mwezi Septemba.
Siku chache zilizopita, Wenger, aliyemtarajia Welbeck arudi kucheza baada ya Krismasi, alisema mchezaji huyo hayuko karibu kurejea uwanjani na huenda wakasubiri hadi Februari.

No comments:

Post a Comment