Mamlaka imepokea malalamiko mengi kuhusu
ucheleweshwaji wa mafao kwa Wanachama jambo ambalo ni kinyume cha Sheriaya
Mamlaka Na. 8 ya mwaka 2008 iliyorekebishwa na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2012
pamoja na Sheria zote za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mamlaka inapenda kuufahamisha Umma
hususan wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwamba kwa mujibu waKifungu cha
35 cha Sheria ya Mamlaka, kulipwa mafao ni haki ya Mwanachama pale
anapokidhi vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria.
Pia ana haki ya
kulipwa mafao yake kwa wakati.Hivyo, Mamlaka inakemea vikali tabia iliyozuka ya
kuchelewesha mafao kwa Wanachama kwa kisingizio cha kutopekea michango toka kwa
Waajiri. Ifahamike kwamba ni jukumu la Mfuko husika kwa mujibu wa Sheria
kukusanya michango toka kwa Waajiri. Jukumu hili si la mwanachama.
Aidha, Mamlaka inapenda Umma ufahamu
kuwa Sheria zote za Mifuko zimeainisha wajibu wa kila Mfuko kulipa mafao kwa
wakati. Vile vile Mfuko unapochelewesha mafao kwa Mwanachama aliyekidhi vigezo
unapaswa kumlipa Mwanachama Tozo kwa
kiwango cha asilimia 15 kwa kila kiasi cha Mafao kilichocheleweshwa.
Hivyo, kwa mujibu wa kifungu cha 6(2),
kupitia Waraka wa Mamlaka Na.1 wa Mwaka 2016 Mamlaka imeielekeza Mifuko yote
kama ifuatavyo:
(1) Kulipa mafao kwa wanachama wote
waliokidhi vigezo kwa wakati.
(2) Kuwalipa wanachama wote ambao mafao
yao yamecheleweshwa kwasababu yoyote ile; Malipo haya yafanyike ndani ya kipindi
cha siku 21 kuanzia tarehe ya taarifa hii.
Imetolewa
na:
Mkurugenzi
Mkuu
Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii – SSRA
S.L.P
31846
Dar
es Salaam

Thanks for sharing, nice post! Post really provice useful information!
ReplyDeleteGiaonhan247 chuyên dịch vụ gửi hàng đi Úc, mua hộ vòng tay pandora úc ship về Việt Nam uy tín và dịch vụ vận chuyển hàng đi campuchia uy tín và kinh nghiệm cách order taobao về VN giá rẻ.