TANGAZO


Sunday, January 31, 2016

SSRA yatoa Taarifa ulipaji wa mafao kwa wanachama wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii


Mamlaka imepokea malalamiko mengi kuhusu ucheleweshwaji wa mafao kwa Wanachama jambo ambalo ni kinyume cha Sheriaya Mamlaka Na. 8 ya mwaka 2008 iliyorekebishwa na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2012 pamoja na Sheria zote za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Mamlaka inapenda kuufahamisha Umma hususan wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwamba kwa mujibu waKifungu cha 35 cha Sheria ya Mamlaka, kulipwa mafao ni haki ya Mwanachama pale anapokidhi vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria. 

Pia ana haki ya kulipwa mafao yake kwa wakati.Hivyo, Mamlaka inakemea vikali tabia iliyozuka ya kuchelewesha mafao kwa Wanachama kwa kisingizio cha kutopekea michango toka kwa Waajiri. Ifahamike kwamba ni jukumu la Mfuko husika kwa mujibu wa Sheria kukusanya michango toka kwa Waajiri. Jukumu hili si la mwanachama.

Aidha, Mamlaka inapenda Umma ufahamu kuwa Sheria zote za Mifuko zimeainisha wajibu wa kila Mfuko kulipa mafao kwa wakati. Vile vile Mfuko unapochelewesha mafao kwa Mwanachama aliyekidhi vigezo unapaswa kumlipa  Mwanachama Tozo kwa kiwango cha asilimia 15 kwa kila kiasi cha Mafao kilichocheleweshwa.

Hivyo, kwa mujibu wa kifungu cha 6(2), kupitia Waraka wa Mamlaka Na.1 wa Mwaka 2016 Mamlaka imeielekeza Mifuko yote kama ifuatavyo:

(1)  Kulipa mafao kwa wanachama wote waliokidhi vigezo kwa wakati.
(2)  Kuwalipa wanachama wote ambao mafao yao yamecheleweshwa kwasababu yoyote ile; Malipo haya yafanyike ndani ya kipindi cha siku 21 kuanzia tarehe ya taarifa hii.



Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii – SSRA
S.L.P 31846

Dar es Salaam

1 comment:

  1. Thanks for sharing, nice post! Post really provice useful information!

    Giaonhan247 chuyên dịch vụ gửi hàng đi Úc, mua hộ vòng tay pandora úc ship về Việt Nam uy tín và dịch vụ vận chuyển hàng đi campuchia uy tín và kinh nghiệm cách order taobao về VN giá rẻ.

    ReplyDelete