TANGAZO


Friday, January 1, 2016

Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Iddi ajumuika na viongozi wastaafu wa Zanzibar katika Hitma ya Kuwaombea Dua Waumini waliotangulia mbele ya haki

Rais Mstahafu wa Tanzania Mzee Ali Haasn Mwinyi (wa pili kushoto), akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa kwanza kushoto wakijumuika na waislamu katika Hitma ya Kuwaombea Dua Waumini waliotangulia mbele ya haki hapo Msikiti wa Ijumaa Kidombo Kijijini kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Dk. Samlin Amour. Wa kwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kanal Mstaafu Juma Kassim Tindwa, Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania Dr. Moha’d Gharib Bilal na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi. 
Waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka sehemu mbali mbali Nchini wakihitimisha Hitma ya kuwaombea waislamu walitangulia mbele ya haki hapo kwenye Msiki wa Ijumaa Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja Kijiji alipozaliwa Rais Mstahafu wa Zanzibar Dr. Salmin Amour. 
Rais Mstahafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Dr. Salmin Amour kati kati akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais Mstahafu wa Tanzania Dr. Moh’d Gharib Bilal kushoto na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi nyumbani kwake Kidombo mara baaya ya chakula cha mchana.
Hafla hiyo inayojumuisha mamia ya waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka pembe zote za Unguja huambatana pia na Maulidi ya Kuzaliwa kwa Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Duniani Mtume Muhammad (SAW), wakati wa usiku ukiwa ni utaratibu wa  Dr. Salmin kuandaa ifikapo Mfunguo Sita wa kila mwaka. (Picha zote na Hassan Issa–OMPR – ZNZ)

No comments:

Post a Comment