TANGAZO


Thursday, December 10, 2015

Vijana nchini watakiwa kuendeleza moyo wa kujitolea

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (mwenye shati la drafi) akivaa gloves kabla ya kuanza kufanya usafi katika eneo la Bamaga Manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo aliwaongoza watumishi wa Manispaa ya Kinondoni na Ofisi ya RPC Kinondoni katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli la kutumia siku ya Uhuru kwa kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (mwenye shati la drafi) akiwaongoza baadhi ya watumishi na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni na vijana wa Dar running Club iliyo chini ya RPC wa Kinondoni katika zoezi la kufanya usafi katika eneo la Bamaga hadi Mwenge jana jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (mwenye shati la drafi) akiwaongoza baadhi ya watumishi na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni na vijana wa Dar running Club iliyo chini ya RPC wa Kinondoni katika zoezi la kufanya usafi katika eneo la Bamaga hadi Mwenge jana jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (kushoto) akiongea na Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi  Kinondoni SACP Kamelius Wambura wakati wa zoezi utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli la kutumia siku ya Uhuru kwa kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira jana jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi akiongea na vijana wa Dar running Club iliyo chini ya  Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi  Kinondoni SACP Kamelius Wambura wakati wa zoezi utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli la kutumia siku ya Uhuru kwa kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira jana jijini Dar es Salaam. 
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi  Kinondoni SACP Kamelius Wambura (mwenye viatu vyekundu) akishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira wakati wa zoezi utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli la kutumia siku ya Uhuru kwa kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira jana jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Kinondoni wakifanya usafi katika Barabara ya Bamaga –Mwenge ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli la kutumia siku ya Uhuru kwa kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira jana jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)

Na Frank Shija,WHVUM
10/12/2015

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bwana James Kajugusu wakati alipowaongoza watumishi wa Manispaa ya Kinondoni katika zoezi la usafi wa mazingira ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli la kuadhimisha siku ya uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira.

“wito wangu ni kwa jamii hasa vijana wajenge moyo wakujitolea kama ambavyo imeonekana leo tabia hii mkiiendeleza italeta manufaa kwenu” Alisema Kajugusi.

Kajugusi aliongeza kuwa mwitikio wa vijana katika zoezi hili ni dhahiri kwamba vijana wameanza kujitambua hivyo ni wajibu wao kujenga na kuiendeleza tabii hii ya kujitolea.

Aidha ametoa wito kwa jamii kutowatenga vijana badala yake iwaone kuwa ni kundi muhimu miongoni mwa jamii ambalo likiongozwa vyema litasaidia katika kuleta tija na manufaa kwa umma na familia zao.

Kwa upande wake mmoja wa kijana aliyeshiriki katika zoezi hilo Bi. Esther Mvile alisema kuwa inawatia moyo kuona viongozi wenye dhamana kubwa nao bila kujali vyeo vyao wameshiriki katika kusafisha mazingira.


Aliongeza kuwa wao kama vijana wamehamasika kushiriki katika zoezi la usafi kutokana na hari aliyoionyesha Mheshimiwa Rais Magufuli katika utendaji wake kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani hivyo tumeshawishika kumuunga mkono na hatutaishi hapa tu.

No comments:

Post a Comment